Na Prince Akbar
KAMATI ya
Uchaguzi ya Chama cha Waliku wa Mpira wa Miguu (TAFCA) imetangaza matokeo ya usaili
wa wagombea uongozi chama hicho, ikiwa imepitisha wagombea sita sita na
kuwaengua wagombea watano kwenye nafasi tofauti.
Baada ya
usaili wa wagombea hao, Kamati ya Uchaguzi ya TAFCA iliwaengua wagombea hao
watano kwa kutokidhimasharti ya Ibara ya 26 (2) ya Katiba ya TAFCA na Kanuni ya
9 ya Kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa TFF na pia kutokidhi utashi wa masharti
ya 11 (1) ya kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa TFF.
Katika
nafasi ya mwenyekiti Oscar Don Korosso alipitishwa kuwa mgombea pekee baada ya
Kenedy Mwaisabula na Jamhuri Kihwelo kuenguliwa kwa kutokidhi masharti ya ibara
ya 26 (2) ya Katiba ya TAFCA na kanuni ya tisa ya Kanuni za Uchaguzi za
Wanachama wa TFF.
Katika
nafasi ya makamu mwenhyekiti, Kamati imempitisha Lister J. Manyara kuwa mgombea
pekee wa nafasi hiyo huku Marco Bundara akipitishwa kuwa mgombea pekee wa
nafasi ya katibu mkuu wa TAFCA.
Hali
kadhalika wagombea wawili wa nafasi ya mjumbe wa mkutano mkuu wa TFF, Wilfred
Kidau na Magoma Rugora wamekidhi masharti ya Katiba ya TAFCA na Kanuni za
Uchaguzi za Wanachama wa TFF na hivyo watachuana kuwania kura za wajumbe wa
mkutano mkuu, huku Ally A Mtumwa
akienguliwa kwa kutokidhi masharti ya kanuni ya 11 (1) ya Kanuni za Uchaguzi za
Wanachama wa TFF.
Katika
nafasi ya ujumbe wa Kamati ya Utendaji, wagombea wote wawili, Abubakar
Balingula na Aboubakar Salum wameenguliwa kwa kutokidhi masharti ya Ibara ya 26
(2) ya Katiba ya TAFCA na Kanuni ya 9 ya Kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa
TFF.