TAARIFA KWA WANAYANGA.
Klabu ya Young Africans ilikuwa ifanye mkutano Wanachama tarehe 08 Disemba 2013, kama ilivyokua imetangazwa na Uongozi hapo awali. Tunapenda kutoa taarifa kuwa tarehe ya mkutano huo sasa imebadilishwa na kusogezwa mbele hadi tarehe 19 Januari 2013 kwa sababu zifuatazo:
1.Kutoa nafasi kwa Wanachama na Wapenzi wa YANGA kushirki kikamilifu maandalizi ya sherehe za Uhuru wa Taifa letu zitakazofanyika tarehe 09, Disemba 2012, na
2.Tuko katika mazungumzo na Kampuni moja maarufu ya kusimamia shughuli za mkutano huo kwa upande wa ufadhili, ili kuweza kutunisha mfuko na Klabu kujiingizia mapato kati ya shilingi za Kitanzania 200,000,000/= (shilingi milioni mia mbili tu) hadi 350,000,000/= (shilingi milioni mia tatu hamsini tu) na Kampuni husika wameomba kuongezewa muda ili waweze kufanya hiyo kwa ufanisi mkubwa.
Tunapenda kuwashukru Wanachama na Wapenzi wa YANGA kwa mshikamano na umoja uliopo. Tuzidi kuijenga Yanga kwa maendeleo na mafanikio daima.
"YANGA DAIMA MBELE, NYUMA MWIKO"
YUSUF MEHBUB MANJI
MWENYEKITI
YOUNG AFRICANS SPORTS CLUB