• HABARI MPYA

    Saturday, April 18, 2009

    YANGA WAHAMISHIA KAMBI DAR


    NYASI za Uwanja wa Taifa wa Dar es Salaam, zinatarajiwa kuwaka moto kesho, wakati miamba miwili ya soka Tanzania, Simba na Yanga, zenye maskani yao eneo la Kariakoo, zikiishi mitaa tofauti, zitakapokuwa zikimenyana katika mchezo wa marudiano Ligi Kuu ya soka ya Vodacom Tanzania Bara.Yanga, wanaoishi makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani, leo watatokea hoteli ya Protea mjini Dar es Salaam, walipohamia leo wakitokea Millennium Sea Breeze Resort, iliyopo Bagamoyo mkoani Pwani, kuingia Uwanja wa Taifa, kumenyana na mahasimu wao wa jadi, Simba, waishio Mtaa wa Msimbazi, ambao nao watashuka dimbani wakitokea katika hoteli ya Bamba Beach, iliyopo Kigamboni, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.Simba, inayonolewa na kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Zambia, Patrick Phiri, mchezo huu unaonekana kuwa muhimu zaidi kwao kushinda, ili pamoja na kulipa kisasi cha kufungwa 1-0 kwenye mchezo wa kwanza, pia kukusanya pointi za kujihakikishia nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu.Kwani tayari Yanga wamekwisha kutwaa ubingwa wa ligi hiyo hata kabla hawajacheza mechi tano za mwisho na sasa Simba inapiga kasia kuwahi kushika tiketi ya kucheza michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika mwakani, ikikimbizwa na Kagera Sugar ya Bukoba na Mtibwa Sugar ya Morogoro.Simba itashuka dimbani kesho, ikiwa na kumbukumbu nzuri ya kushinda mechi zake mfululizo, dhidi ya Kagera Sugar 2-0, Azam FC 3-0 na Toto Afrika 1-0, wakati Yanga katika mechi zake tatu zilizopita, ilifungwa moja na Azam FC 3-2, sare moja na Kagera Sugar na kushinda moja dhidi ya wachovu, Polisi Dodoma.Yanga ilicheza na Kagera, Azam na Polisi tayari ikiwa bingwa, baada ya kuifunga Toto 2-1 mjini Mwanza, hivyo inawezekana haikucheza kwa kiwango chake halisi, lakini leo kulingana na uzito wa mchezo huu, hapana shaka watacheza kama wanatafuta taji. Akizungumza na bongostaz leo, kwenye kambi ya klabu hiyo, Kocha wa Simba, Patrick Phiri, alisema kwamba timu yake ina mifumo miwili, ambayo ni 4-4-2 na 4-5-1, hivyo katika mchezo wa leo wataamua waanze na upi na wanaweza kubadilisha kulingana na wapinzani wao watakavyokuwa.ÒMara nyingi mifumo ni ile ile, ila inategemeana na malengo yako, wengine wanakuwa na malengo ya kuanza kwa kushambulia, wengine kuanza kwa kuzuia, sisi tutaanza kwa kuwasoma kwanza wapinzani wetu kujua wanataka nini,Ó alisema Phiri.Winga huyo wa zamani wa timu ya Taifa ya Zambia, alisema kwamba kwa sababu Yanga tayari ni mabingwa, wanaweza kuamua kuutumia mchezo huo kuchezea mipira tu kwa lengo la kupoteza muda, kwa sababu hawana cha kupoteza zaidi ya kulinda heshima.ÒLakini sisi tunataka kushinda ili tupunguze shinikizo katika mechi inayokuja (dhidi ya Polisi mjini Dodoma), tukifungwa na Yanga, tutaendelea kuwa na mchecheto katika mechi inayokuja, tunataka tushinde ili na sisi tucheze mechi ya mwisho, kama wenzetu Yanga watakavyocheza na sisi,Ó alisema.Kuhusu kikosi chake cha kwanza kwenye mchezo wa leo, Phiri alisema kwa utamaduni wa Simba na Yanga ni vigumu kutaja. Hata hivyo, kuna uwezekano langoni akaanza Ally Mustafa ÔBarthezÕ, kulia anaweza kuanza Salum Kanoni kwa sababu Anthony Matangalu ni majeruhi, kushoto Juma Jabu. Katikati kwa sababu Meshack Abel hayuko vizuri kimchezo, wanaweza wakasimama Juma Nyosso na Kelvin Yondani, wakati mbele yao anaweza kuwapo Henry Joseph, pembeni kulia Nico Nyagawa, kushoto Ulimboka Mwakingwe na kiungo wa mbele huenda akasimama Jabir Aziz, wakati washambuliaji wanaweza kuanza Haruna Moshi na Emeh Izuchukwu.Wachezaji wa akiba wanaweza kuwapo Deo Munishi ÔDidaÕ, Ramadhan Wasso, Abel, David Naftari, Ramadhan Chombo ÔRedondoÕ, Mohamed Banka, Adam Kingwande, Mohamed Kijuso na George Nyanda.Kwa upande wa Yanga, akizungumza jana kwenye kambi ya timu hiyo, kocha wa timu hiyo, Profesa Dusan Kondic, alisema kwamba wako vizuri na tayari kwa mchezo huo, ambao aliuita wa maonyesho.Alisema anawaheshimu Simba ni timu nzuri na inacheza kwa lengo la kupata kitu, lakini kulingana na historia ya timu hizi, vijana wake wamepania kuwasimamisha hii leo.ÒWao wanataka nafasi ya pili, wanacheza kwa hamasa, sisi kwetu hatuna cha kupoteza na tupo kwa ajili ya kukamilisha ratiba ya Ligi na kufunga msimu kwa furaha, hatutakuwa tayari kupoteza mchezo,Ó alisema.Ingawa Kondic hakutaja kikosi cha kwanza kwenye mchezo huo, zaidi ya kusema tu langoni atamuanzisha Juma Kaseja, lakini kuna uwezekano kikawa hivi;Kaseja, Nsajigwa Shadrack, Nurdin Bakari, Nadir Haroub ÔCannavaroÕ, Wisdom Ndhlovu, George Owino au Geoffrey Bonny, Shamte Ally, Athumani Iddi ÔChujiÕ, Boniphace Ambani, Ben Mwalala na Mike Barasa au Vincent Barnabas.Wakati huo kwenye benchi watakuwapo Steven Marashi, Abubakar Mtiro, Castory Mumbara, Kiggi Makasy, Abdi Kassim, Razack Khalfan, Jerry Tegete na Maurice Sunguti.Je, nani atacheka, nani atanuna baada ya dakika 90 za mchezo huo utakaochezeshwa na Israel Nkongo? Bila shaka hilo ni jambo la kusubiri na kuona.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA WAHAMISHIA KAMBI DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top