• HABARI MPYA

    Friday, April 24, 2009

    KASEJA: MSINIPELEKE SIMBA JAMANIA, NIPO YANGA


    KIPA mahiri nchini, Juma Kaseja amesema taarifa mbalimbali kuhusiana na usajili wa wachezaji wa Ligi Kuu Tanzania Bara unamweka katika wakati mgumu ndani ya klabu hiyo na kumfanya asiwe na amani. Akizungumza Dar es Salaam jana, Kaseja amesema yeye bado mchezaji halali wa Yanga, lakini wapo baadhi ya watu wamekuwa wakimhusisha na masuala yasiyo na msingi. "Kwa wiki mbili sasa nimekuwa nikihusishwa na masuala ya kuondoka Yanga, mambo ambayo wala hayapo kwa sasa katika mawazo yangu, hata ligi haijamalizika. "Mimi sifanyi uamuzi kwa kufuata watu wanasema nini, sijatofautiana na Yanga, wala sina sababu ya kukurupuka kuondoka, maana mkataba wangu bado karibu mwezi mmoja na nusu," alisema Kaseja. Alisema hivi sasa haamini ndani ya Yanga kwa kuonekana anataka kuondoka na kurejea timu yake ya zamani ya Simba, jambo ambalo amesema halipo mawazoni mwake kwa sasa kwani yeye bado ana mkataba na Yanga. "Wakati nasaini Yanga hakuna aliyejua, mimi ni mtu mzima, nimeishi kwa amani Yanga, lakini siku za karibuni naharibiwa ama na baadhi ya wadau wa Simba au watu wachache ndani ya Yanga," alisema Kaseja. Kipa huyo alilalamika kuwa hata taarifa zinazotolewa na baadhi ya vyombo vya habari zikimhusisha na kutaka kuondoka Yanga, nazo zinamfanya aonekane si mwaminifu kwa mwajiri wake ambaye ni Yanga. "Mkataba wangu unamalizika Juni, tayari nimezungumza na viongozi wangu kwamba mkataba ukiisha au ukikaribia kabisa kuisha tutakaa na kuzungumza, lakini haya yanayoendelea yananifanye nisiwe na amani. "Wapo wasionitakia mema wanadiriki hata kusema nimezungumza na baadhi ya viongozi wa klabu nyingine, kwa kweli ni kutaka kunifukuzisha kwenye klabu yangu na kunigombanisha na viongozi ama wanachama," alisema kipa huyo mahiri nchini. Kipa huyo anahusishwa na kujiunga na Azam FC inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara, au kurejea klabu yake ya zamani ya Simba, ingawa jana alisisitiza mashabiki wamwache na wasimharibie maisha yake. Aliwalaumu baadhi ya viongozi wa mpira kwa kutaka kumtumia yeye kufanikisha mambo yao, ama kudai wanamsajili au wengine kutamka maneno ambayo anaamini yanaweza kuwachochea Yanga kumwona ni msumbufu na asiyekuwa na nidhamu. Kipa huyo alisajiliwa na Yanga Juni mwaka jana kwa Sh milioni 40, huku uhamisho wake pia kutoka Simba ukigharimu karibu Sh milioni 25 IMETOKA GAZETI LA HABARI LEO
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KASEJA: MSINIPELEKE SIMBA JAMANIA, NIPO YANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top