• HABARI MPYA

  Ijumaa, Aprili 10, 2009

  NGASSA: NITAJITUMA KWA BIDII YANGU YOTE


  MRISHO Khalfan Ngassa anayeondoka Jumapili hii kwenda England kufanya majaribio katika klabu ya West Ham United, amesema kwamba atafanya bidii ili kuhakikisha ananunuliwa na klabu hiyo.
  Akizungumza na bogostaz leo, Ngassa amesema kila kitu kipo safi na anakwenda akiwa fiti kimwili na kiakili, hivyo ana matumaini ya kukata kiu yake, ambayo ni kununuliwa na klabu hiyo.
  "Nitajituma kwa bidii yangu yote, nifanya vizuri na nipate mkataba na West Ham,"alisema Ngassa atakayeondoka na wakala wake, Yussuf Bakhresa. bongostaz inamtakia kila heri dogo huyu mwenye kipaji na kasi uwanjani kama Gianfranco Zola enzi zake, ambaye sasa anaifundisha West Ham. (Pichani Ngassa akiwa na kocha Msaidizi wa Taifa Stars, Ally Bushiri)
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: NGASSA: NITAJITUMA KWA BIDII YANGU YOTE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top