• HABARI MPYA

  Jumamosi, Aprili 18, 2009

  KONDIC AMPA DARASA KASEJA

  Kaseja kwenye basi la Yanga wenzake baada ya mazoezi


  KOCHA Mkuu wa klabu ya Yanga ya Dar es Salaam, Profesa Dusan Kondic, amesema kipa Juma Kaseja anapaswa kutumia vizuri mchezo wa kesho dhidi ya mahasimu wao wa jadi, Simba kwa kudaka vizuri ili kudhihirisha ubora wake na kujitengenezea mazingira ya kurejeshwa timu ya taifa, Taifa Stars.Akizungumza na bongostaz jana kwenye kambi ya Yanga, Millennium Sea Breeze Resort, Bagamoyo mkoani Pwani, Kondic alisema kwamba Kaseja ni kipa bora Tanzania, katika hilo hakuna ubishi, hivyo Jumapili ni siku ya kudhihirisha ubora wake. Hata hivyo Yanga ilihama jana kutoka Bagamoyo, hadi Protea Hotel, Dar es Salaam.ÒNimeweka matumaini yangu yote kwa Kaseja, ni kipa bora nchi hii, anatakiwa kutumia nafasi hii kuonyesha uwezo wake, kudhihirisha yeye ni bora ili ajitengenezee mazingira ya kurejeshwa timu ya taifa,Ó alisema Kondic.Kuhusu maandalizi ya mchezo huo kwa ujumla, Kondic alisema kwamba ni mazuri na atautumia mchezo huu kujua wachezaji wanaostahili kubaki naye kwenye timu na ambao anapaswa kuwatema.ÒNimewaambia wachezaji, huu ni mchezo wao, wautumie mchezo huu kuniridhisha kwamba wanastahili kuongezwa mkataba, yeyote atakayeboronga, sitakuwa na huruma naye, nitamuambia asante na kwaheri,Ó alisema Kondic.Mserbia huyo alisema kwamba anafahamu kwenye soka lolote linaweza kutokea, lakini Yanga kama mabingwa wanapaswa kuonyesha uwezo wao uwanjani na kudhihirisha ubora wao uliowapa ufalme wa soka nchini kwa mara ya pili mfululizo chini yake.Alisema anashukuru wachezaji wake wako vizuri, hawana mchecheto kwa sababu wanajua hawana cha kupoteza kwenye mchezo huo, hivyo ana matumaini makubwa ya nyota ya Jangwani kungÕara jioni ya kesho.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KONDIC AMPA DARASA KASEJA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top