• HABARI MPYA

    Saturday, April 04, 2009

    MATOLA AMPA VID0NGE MWAKALEBELA

    Matola akiwa na Emanuel Gabriel katikati na Shekhan Rashid kulia enzi zao Simba SC


    KIUNGO wa zamani wa klabu ya Simba ya Dar es Salaam, Suleiman Abdallah Matola amemtaka Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Frederick Mwakalebela kuwaheshimu wachezaji wa zamani na kuwawekea utaratibu mzuri wa kuingia bure kwenye mechi.Akizungumza na mjini Dar es Salaam, Matola alisema kwamba wapo wachezaji ambao kweli hawakufikia hatua kubwa ya kutoa mchango wao kwa taifa hili, lakini kuna wengine kutokana na uwakilishi wao enzi zao dimbani, ni jambo la aibu kuwazuia japo tu kuingia uwanjani bure.ÒNani asiyeujua mchango wangu kwa taifa hili, kibaya zaidi nilizuiliwa kuingia katika mchezo ambao timu zote nimezichezea, (Simba Vs Azam). Mimi nimecheza Simba kwa mafanikio makubwa, nimenyanyua mataji kibao pale Msimbazi. Nilikuwa nachomwa sindano za ganzi ili niichezee Simba.Hiyo Azam inacheza Ligi Kuu msimu huu, mimi ndio nimeipandisha na baada ya hapo nikaamua kuachana na mpira. Lakini eti nazuiliwa kuingia, tena nazuiliwa na mtu ambaye ananijua fika na anautambua mchango wangu katika soka ya nchi hii, Msafiri Mgoyi (Mjumbe wa TFF, anajulikana kama Ahmad Mgoyi).Kwa kweli kimeniuma sana, na si mimi eti hata Edibily (Lunyamila) anazuiliwa kuingia uwanjani? Hii kwa kweli Mwakalebela lazima aelewe hatutendei haki wachezaji ambao tumeifanyia mambo makubwa nchi hii,Óalisema Matola.Kiungo huyo alisema kwamba TFF inapaswa kuwawekea utaratibu maalum wachezaji wa zamani ambao wamo kwenye rekodi za kitaifa, kwenda kuchukua tiketi za kuingia uwanjani bure, kwani anaamini utaratibu huo upo duniani kote.ÒHii timu ya taifa ya Tanzania, sizungumzii ya Bara, nasema Taifa Stars, katika historia yake imetwaa Kombe moja tu, Kombe la Castle, mimi nilikuwa miongoni mwa nyota walioiwezesha timu hii kutwaa lile Kombe pale Mwanza (mwaka 2001), leo unanizuia kuingia uwanjani, ni haki kweli hii?Óalihoji Matola. Katika michuano hiyo, Stars iliyokuwa chini ya Mkurugenzi wa Ufundi Mjerumani Burkhad Pape na makocha Charles Boniphace Mkwasa na Syllersaid Kahema Mziray, ilianza kuitoa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kwa mikwaju ya penalti 4-2, baada ra sare ya 2-2.Shujaa wa mchezo huo, alikuwa Nteze John Lungu aliyeifungua Stars bao la kusawazisha dakika ya 88, baada ya DRC kutoka nyuma kwa 1-0 na kuongoza 2-1 kutokana na mabao ya Dikilu Bageta dakika ya 44 na Kasongo Bukasa dakika ya 67. Nteze pia ndiye aliyeifungia Stars bao la kuongoza dakika ya 10, Uwanja wa Sheikh Amri Abedi mjini Arusha.Katika fainali iliyopigwa Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza, Stars iliitandika Kenya, Harambee Stars mabao 3-1, wafungaji wake wakiwa ni Yussuf Macho Rwenda dakika ya 26, Emmanuel Gabriel Mwakyusa dakika ya 66 na Salvatory Edward Agustino dakika ya 90, wakati wageni walipata la kufutia machozi kupitia kwa Robert Mambo dakika ya 85.Kikosi cha kwanza cha Stars kwenye michuano hiyo kilikuwa Peter Manyika, Mecky Maxime, Alphonse Modest, Boniface Pawasa, John Mwansasu, Suleiman Matola aliyekuwa akimpisha Waziri Mahadhi, Saidi Maulid 'SMG', Yussuf Macho, Salvatory Edward, Emmanuel Gabriel aliyekuwa akimpisha Joseph Kaniki na Nteze John.Wachezaji wengine waliokuwepo kwenye timu hiyo ni Mengi Matunda, Juma Kaseja, Kassim Issa, Qureish Ufunguo, Abubakar Mkangwa, Primus Kasonzo, Faustine Lukoo, Rajab Shamte, Sostenes Manyasi na Edibily Lunyamila.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MATOLA AMPA VID0NGE MWAKALEBELA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top