• HABARI MPYA

  Jumapili, Aprili 05, 2009

  SIMBA YAKAMATA NAFASI YA PILI


  MABAO mawili yaliyofungwa na mshambuliaji Mnigeria, Emeh Ezuchukwu (pichani) jana yaliipa Simba ushindi 2-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya wenyeji Kagera Sugar, kwenye Uwanja wa Kaitaba, Bukoba.
  Kwa ushindi huo, Simba imetimiza pointi 33 baada ya kucheza mechi 19 hivyo kukalia nafasi ya pili kwenye ligi hiyo, ambayo tayari ubingwa wake umekwishachukuliwa na Yanga.
  Kagera imeporomoka hadi nafasi ya nne sasa, kwani Mtibwa Sugar iliyoshinda 3-0 dhidi ya Moro United imepanda hadi nafasi ya tatu kwa pointi zake 31.
  Kagera ikmebaki na pointi zake 28 na sasa ina kazi kubwa ya kuhakikisha inashinda mechi zake zote zilizosalia ili kupigania nafasi ya pili, huku pia ikiziombea dua mbaya Simba na Mtibwa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  1 maoni:

  Item Reviewed: SIMBA YAKAMATA NAFASI YA PILI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top