• HABARI MPYA

  Alhamisi, Aprili 16, 2009

  REDD'S ORIGINAL KUDHAMINI UREMBO DAR

  Meneja Masoko wa TBL, David Minja


  KAMPUNI ya Bia Tanzania (TBL), kupitia kinywaji chake cha Redd’s wametangaza udhamini wa mashindano ya urembo katika ngazi ya kanda na vitongoji nchini utakaogharimu zaidi ya Sh milioni 200. Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Meneja wa kinywaji cha Redds Premium Cold, Kabula Nshimo, alisema TBL wameamua kujikita kuanzia mashindano ya kanda na vitongoji mwaka huu, ili kuweka mizizi kuelekea kwenye shindano la taifa la Miss Tanzania 2009. Alisema kwa miaka kadhaa TBL kupitia Redd’s wamekuwa wakidhamini washiriki wa shindano Miss Tanzania katika kutafuta Balozi mwanamitindo wa Redds na sasa wameamua kuweka jitihada zao kuanzia kwenye mizizi. “Tayari tumefikia makubaliano ya kudhamini mashindano ya kanda ya Ilala, Temeke na Kinondoni kwa mkoa wa Dar es Salaam, hatutaishia hapo pia tutadhamini mashindano ya kanda nyingine, mikoani na vitongoji. “Lakini bado tunaendelea na mazungumzo na waandaaji wa Miss Tanzania kuangalia udhamini wetu mwaka huu na baada ya mazungumzo kukamilika tutawaita na kuwafahamisha,” alisema.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: REDD'S ORIGINAL KUDHAMINI UREMBO DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top