• HABARI MPYA

  Alhamisi, Aprili 02, 2009

  VIINGILIO YANGA VS AL AHLY HIVI HAPA


  SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limetangaza viingilio vya mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Yanga na Al Ahly ya Misri itakayofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Jumamosi.
  Kiingilio cha juu katika mchezo huo, kimepangwa kuwa Sh30,000 kwa VIP A wakati VIP B ni Sh20,000 na VIP C kiingilio kitakuwa Sh10,000. Viti vya rangi ya chungwa ni Sh5,000 wakati viti vya rangi ya bluu na kijani ni Sh3,000.
  Ofisa Habari wa TFF, Florian Kaijage alisema, baada ya kukutana na uongozi wa Yanga, juzi na jana walikubaliana kimsingi na hata kuandika barua Shirikisho la Soka Afrika, CAF na Chama cha Soka Misri kuwataarifu juu ya mabadiliko ya uwanja.
  Awali, Yanga walipanga kutumia Uwanja wa Uhuru kwa mchezo huo, kabla ya kupituishwa uamuzi wa kutumia Uwanja wa Taifa. Kwa uamuzi huo wa kubadilisha uwanja, Yanga italazimika kulipa CAF, dola 2,000.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: VIINGILIO YANGA VS AL AHLY HIVI HAPA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top