• HABARI MPYA

  Saturday, April 18, 2009

  TEGETE AIOKOA YANGA KUZAMA KWA SIMBA


  BAO lililofungwa na mshambuliaji wa timu ya Taifa na klabu ya Yanga, Jerry Tegete katika dakika za lala salama za mchezo ziliiwezesga timu ya Yanga kutoa sare ya mabao 2-2 na watani wao wa jadi Simba. Katika mchezo huo uliofanyika jana kwenye uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam Simba ndio walikuwa wa kwanza kupata bao katika kipindi cha kwanza lililofungwa kwa kichwa na mshambuliaji Ramadhan Chombo ‘Redondo’ katika dakika ya 23. Chombo alifunga bao hilo kwa kumalizia vema mpira wa juu wa adhabu uliopigwa pembeni mwa lango la Yanga na Henry Joseph na kumfikia na kuruka kichwa ambacho kipa Juma Kaseja wa Yanga alichupa hewani katika harakati za kuokoa lakini juhudi hizo zilishindikana na mpira kutumbikia wavuni. Yanga ambao walianza mchezo huo kwa kasi na kuanza na kupata kona ya kwanza mapema katika dakika ya kwanza ya mchezo iliyotokana na krosi ya Mike Baraza iliyoleta kizazaa kwenye lango la Simba na kumkuta Ben Mwalala lakini beki Juma Jabu aliwahi na kutoa mpira huo kona kabla ya Mwalala hajaleta madhara. Dakika ya nane Yanga tena walibisha hodi langoni mwa Simba pale Amir Maftah alipogongena vema na Godfrey Bonny ambye alitoa krosi ambayo Jabu aliikoa kabla ya kumfikia Boniface Ambani. Baada ya mashambulizi hayo Simba ilizinduka na katika dakika ya tisa mpira wa adhabu uliopigwa na Joseph uliokuwa ukielekea wavuni uliokolewa kiustadi na Kaseja na kuwa kona, adahabu hiyo ilitokana na beki Shadrack Nsajigwa kumchezea vibaya Ulimboka Mwakingwe. Simba iliendelea kulisakama lango la Yanga huku wakionana kwa kucheza pasi fupifupi za uhakika dakika ya 16 mlinzi Juma Said ‘Nyoso’ alipenyeza pasi safi ndani ya eneo la hatari la Yanga na kumkuta Mwakingwe ambaye alipiga shuti kali na Kaseja kulipangua na kumkuta Redondo aliyeshindwa kutumbukiza mpira huo wavuni akiwa kwenye nafasi nzuri kwani shuti lake lilipaa juu ya lango. Simba tena ilipoteza nafasi nyingine nzuri katika dakika ya 27 pale Boban alipomtoka Maftah na kupiga krosi ndani ya eneo la hatari lakini Mwakingwe akiwa kwenye nafasi nzuri ya kufunga anashindwa kuunganisha pasi hiyo ambayo inaokolewa na Wisdom Ndhlovu na kuwa kona ambayo iluokolewa na Kaseja. Dakika Yanga walimtoa Athumani Iddi ‘Chuji’ ambaye alikuwa nahodha kwenye mchezo huo alitolewa baada ya kuonekana kupwaya katika kipindi cha kwanza na nafasi yake ilichukuliwa na Nurdin Bakari Pamoja na timu zote kuonyesha soka nzuri mwamuzi Israel Nkongo pamoja na wasaidizi wake walishindwa kumudu mchezo huo na kusababisha kutoa maamuzi yalikuwa yakipingwa ama na wachezaji au mashabiki waliofurika kiwanjani kushuhudia pambano hilo. Hadi kufikia kipindi cha mapumziko Simba walikuwa mbele kwa bao 1-0 Kipindi cha pili Yanga ilikianza kwa kasi na dakika tatu tu mara baada ya kuanza mchezo huo mshambuliaji wa timu hiyo Mwalala ambaye katika mchezo wa raundi ya kwanza ndie alifunga bao pekee la ushindi la timu hiyo alipachika bao la kusawazisha kirahisi baada ya mpira was krosi uliokolewa na kipa Mustafa Ali wa Simba kumfikia. Baada ya bao hilo timu zote zilicheza kwa kushambuliana kwa zamu na katika dakika ya 62 , Haruna Moshi ‘Boban’ ambaye pia alichaguliwa kuiwa mchezaji bora wa mechi hiyo na kuzawadiwa sh laki tatu na Voadacom ambao ni wadhamini wa ligi hiyo aliifungia Simba bao la pili baada ya kumaliza mpira uliookolewana walinzi wa Yanga na kumfika. Kuona hivyo Yanga iliwatoa Boniface Ambani kuingia Shamte Ally wakati Simba iliwatoa Mwakingwe na Redondo na kuwaingiza Mohamed Kijuso na Emeh Izuchukwu  PHIRI AMUASA BOBAN
  KUELEKEA kwenye mechi muhimu ya ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara kesho baina ya mahasimu wa jadi katika soka nchini, kocha wa Simba, Patrick Phiri, amemuasa kiungo wake tegemeo, Haruna Moshi ÔBobanÕ kujiepusha na hasira.Akizungumza na bongostaz jana katika kambi ya timu hiyo iliyopo Bamba Beach, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, Phiri alisema mara kadhaa amezungumza na mchezaji huyo kuhusiana na hasira zake na inampa moyo kwamba sasa amebadilika kwa kiasi kikubwa.ÒHaruna amebadilika sana, nadhani utoto pia ulichangia tabia yake. Lakini ana tofauti kubwa na ukizingatia pia ameshawahi kwenda kucheza Uarabuni kwa mwaka mmoja, ni lazima atakuwa amepata uzoefu wa kutosha.ÒHata ukimuona anavyocheza hivi sasa, ametulia sana, hachezi rafu na si mkorofi, nafikiri maneno yangu yamemuingia na yamemsaidia. Lakini pia siyo Haruna tu, hata wachezaji wengine nao tunakaa nao na kuwaeleza madhara ya hasira kwa sababu yanaigharimu timu kutokana na umuhimu wao kikosini,Ó alisema.Phiri alisema wachezaji wake wote wapo katika hali nzuri kiafya, isipokuwa Antony Matangalu, ambaye alipata maumivu ya kifundo cha mguu, hali ambayo inamfanya kucheza kwake kutegemee maoni ya daktari wa timu hiyo.Kuhusu kutocheza kwa kipindi kirefu kwa mlinda mlango Amani Simba, alisema mchezaji huyo alikuwa na ruhusa maalumu ya kwenda kuoa na kwamba amerejea siku chache zilizopita, ingawa alikataa kwamba hamchezeshi.ÒTuna makipa watatu na wote wanapewa nafasi, Dida alidaka, Amani alidaka na Mustapha alidaka, kwa hiyo utaona kwamba kila mmoja amepata nafasi kuonyesha uwezo wake,Ó alisema.Ingawa alikataa kutaja kikosi kitakachoanza kwa maelezo kuwa ni sawa na kuonyesha silaha kwa adui, lakini kwa mwenendo wa hivi karibuni wa kikosi hicho, pamoja na hali ya kambi ilivyo, huenda kikosi cha kwanza kikawa hivi:Ally Mustapha ÔBathezÕ, Salum Kanoni, Juma Jabu, Juma Nyosso, Kelvin Yondani, Henry Joseph, Nico Nyagawa, Jabir Aziz, Emeh Ezuchukwu, Haruna Moshi na Ulimboka Mwakingwe.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TEGETE AIOKOA YANGA KUZAMA KWA SIMBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top