• HABARI MPYA

  Jumamosi, Aprili 18, 2009

  NGASSA MAMBO SAFI UK, AITAKIA HERI YANGA


  PAMOJA na kuitakia heri Yanga kwenye mchezo wake wa leo dhidi ya watani wao wa jadi, Simba, winga wa klabu hiyo, Mrisho Ngassa (pichani), amesema kwamba kesho ndiyo atajua mustakabali wake wa majaribio katika klabu ya West Ham United nchini England.
  “Watakaa Jumapili kufanya tathmini zao, natarajia Jumatatu wakala wangu (Yussuf Bakhresa) atapewa jibu kama inakuwaje kuhusu mimi,” alisema Ngassa, alipozungumza na DIMBA kwa simu kutoka Upton Park, Mashariki mwa London, ambako yuko chini ya Gianfranco Zola, kocha wa West Ham akijaribiwa.
  Ngasa alipofika mjini humo alianza kufanya mazoezi na wachezaji waliokwenda kwenye majaribio, baadaye akahamishiwa kwenye wachezaji wa akiba wa klabu hiyo na Alhamisi alianza kufanya mazoezi na kikosi cha kwanza cha West Ham.
  “Mimi namshukuru Mungu naona kama mambo yanakwenda vizuri, sitakuwa na mazoezi tena hadi hiyo Jumatatu, siku ambayo ndio nitapata jibu,” alisema Ngassa na kuongeza.
  “Zaidi nawatakia wenzangu kila la heri katika mechi na Simba, nawaombea washinde, kama wao wanavyoniombea dua nifanikiwe huku, na mimi nawaombea dua washinde hiyo mechi,” alisema.Ngassa aliondoka nchini Jumapili kwenda Uingereza kufanya majaribio ya kujiunga na klabu ya West Ham United, ambayo imeonekana kuanza kuvutiwa naye
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: NGASSA MAMBO SAFI UK, AITAKIA HERI YANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top