• HABARI MPYA

  Jumanne, Aprili 14, 2009

  MTIBWA YAIPA AHUENI SIMBA


  MSHAMBULIAJI Abdallah Juma leo ameendeleza cheche zake za ufungaji mabao, baada ya kuifungia Mtibwa Sugar bao la kusawazisha dakika 20 ilipokuwa ikimenyana na Total Africa ya Mwanza iliyotangulia kupata bao dakika ya nane, hivyo kufanya sare ya 1-1
  Mchezo huo ulichezwa kwenye Uwanja wa Manungu, Turiani mjini Morogoro na wenyeji walimlalamikia mwamuzi kuwanyima mabao mawili yaliyofungwa na Rashid Gumbo na Kassim Issa.
  Kwa sare hiyo Mtibwa imebaki kwenye nafasi ya tatu ikiwa na pointi 32, ikiwa ni pointi nne nyuma ya Simba ambayo iko nafasi pili ikiwa na pointi 36. Mtibwa sasa inahitaji kushinda mechi zake mbili zilizobaki huku ikiombea dua mbaya Simba, ili iweze kumaliza katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi. Mshindi wa pili, huiwakilisha nchi kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho linaloandaliwa na Shirikisho la Soka la Afrika (CAF). Katika mchezo mwingine, Azam ililazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na wenyeji Kagera Sugar mjini Bukoba.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MTIBWA YAIPA AHUENI SIMBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top