• HABARI MPYA

  Friday, April 10, 2009

  MARSH: HAKUNA WA KUFURUKUTA TENA KWA AZAM


  KOCHA wa Azam FC, Sylvester Marsh aliyechukua mikoba kuinoa timu hiyo baada ya kutimuliwa kwa Neider dos Santos, amesema hivi sasa wanahitaji kushinda zaidi ili kujitengenezea mazingira mazuri ya kubaki Ligi Kuu msimu ujao.
  Azam hivi sasa imefikisha pointi 25 sawa na Toto African baada ya juzi kuichapa Yanga mabao 3 - 2.
  Mash alisema wanahitaji kushinda michezo yao yote iliyobaki ili waweze kutuliza akili na kupanga mambo mapya ya msimu ujao wa Ligi.
  "Ujue kwenye soka lolote linaweza kutokea hivyo ni lazima tukaze buti, unaweza ukasema nitabaki kwenye ligi lakini gafla upepo ukabadilika ukashangaa unashuka.
  "Maadamu tumeshinda mechi hii naamini tuna uwezo wa kushinda mechi nyingine zijazo ili tujihakikishie nafasi kamili ya kubaki kwenye ligi na tuendelee na mipango mingine.
  Alisema ushindi wa mechi dhidi ya Yanga umechangiwa na kujituma kwa wachezaji ambao walikuwa wamepania ushindi.
  "Kipindi cha kwanza tulizidiwa lakini kipindi cha pili wachezaji wangu walibadilika na kuweza kucheza vizuri hivyo kutupa ushindi huo najua Yanga walishadhani wamemaliza baada ya kuongoza kwa mabao 2 - 0 lakini kwenye mpira hutakiwi kuwa hivyo, unapambana mpaka filimbi ya mwisho ya mwamuzi" alisema Mash.
  Azam imebakiza michezo mitatu dhidi ya Kagera Sugar, Prisons na Toto African. (Pichani kushoto ni Marsh akiwa Marcus Tinocco, Mbrazil aliyekuwa kocha wa timu za taifa za vijana Tanzania)
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MARSH: HAKUNA WA KUFURUKUTA TENA KWA AZAM Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top