• HABARI MPYA

  Monday, April 13, 2009

  AMBANI ANATAKA BAO NNE MECHI MBILI
  MSHAMBULIAJI wa klabu ya Yanga ya Dar es Salaam, Boniphace Ambani (pichani kulia akisalimiana na Blatter rais wa FIFA) amesema anataka kufunga mabao yasiyopungua manne katika mechi tatu za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania zilizobakia kuanzia Jumapili ijayo dhidi ya Simba na Aprili 26 dhidi ya Villa Squad, zote Jijini.
  Ambali aliiambia bongostaz mjini Dar es Salaam kwamba, anataka kufunga mabao hayo ili atimize mabao 20 baada ya Ligi Kuu na kutwaa tuzo ya mfungaji Bora wa ligi hiyo kwa madaha zaidi.
  “Kwangu kila bao nalofunga kwenye mechi nahesabu, hicho ndio kitu ambacho kinaniweka kwenye chati ya ufungaji, kufunga kwenye mechi dhidi ya Simba au kutofunga hakutabadilisha kitu,”alisema Ambani.
  Hata hivyo, Ambani aliyeumia na kipigo cha 3-2 kutoka Azam, siku ambayo yeye alijiongezea mabao mawili, alisema: “Nataka kutimiza mabao 20 katika mechi hizi zilizobaki,”alisema.
  Yanga imekwishatwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Bara, kwani hadi sasa ina pointi 47 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote inayoshiriki ligi hiyo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AMBANI ANATAKA BAO NNE MECHI MBILI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top