• HABARI MPYA

    Thursday, September 04, 2014

    FALCAO: RAHA SANA KUWA MAN UNITED, NILIKUWA KWENYE MAZUNGUMZO NAO MUDA MREFU

    MSHAMBULIAJI Radamel Falcao amesema kwamba alikuwa kwenye mazungumzo na Manchester United kwa miezi kadhaa kabla ya uhamisho wake katika siku ya mwisho ya kufunga pazia la usajili.
    Mshambuliaji huyo wa Colombia alihusishwa kwa kiasi kikubwa na kuhamia Real Madrid, kabla uhamisho wake wa ghafla kuelekea Old Trafford. 
    Falcao, akizungumza jana wakati akijiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Brazil mjini Miami usiku wa Ijumaa amesema: "Ninajivunia sana kuwa Manchester United,".
    Tayari kwa kazi: Radamel Falcao (katikati) akijifua na Colombia mjini Miami jana

    "Tumekuwa kwenye mazungomzo na klabu kwa miezi fulani, na mwishowe, tulifikia makubaliano na Monaco katika siku ya mwisho ya kufunga pazia la usajili,".
    Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 alilazimika kusubiri hadi Saa 7.30 Jumanne ili kukamilisha uhamisho wake wa mkopo wa msimu wa Pauni Milioni 6 kutoka Monaco na kuthibitishwa na Ligi Kuu na kuwa mchezaji wa United. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: FALCAO: RAHA SANA KUWA MAN UNITED, NILIKUWA KWENYE MAZUNGUMZO NAO MUDA MREFU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top