• HABARI MPYA

    Wednesday, September 03, 2014

    TFF IMEWAFIKISHA HAPA YANGA NA OKWI, KWA FAIDA YA NANI?

    KATIKA makala yangu iliyopita, nilielezea kwa muhtasari historia ya mchezaji Emmanuel Arnold Okwi kutoka Simba SC, Etoile du Sahel, Yanga SC hadi kurudi Simba SC.
    Juni 27, mwaka huu, Yanga SC waliandika barua TFF kumlalamikia mchezaji huyo na mwishowe wakaomba; “With that said, we request your good office to nullify our agreement with Mr Emmanuel Arnold Okwi and oblig him to refund us the Sinning Fee paid to him as advance and in good faith, refund Yanga salaries wrlongly collected by him and make the player pay damages to the tune of USD 200,000 to the club due for the loss of income and good will for not retaining the Premier League Championship and Mark our Agreement with him as not consummated,” 
    Bila shaka baada ya ukimya wa TFF kutojibu barua hiyo ya
    Juni 27, Yanga wakaandika barua nyingne Agosti 25 ambayo malalamiko dhidi ya mchezaji yaliongezeka.
    Walimlalamikia kuingia kwenye mazungumzo na klabu Wadi Degla ya Misri akiwa bado ana Mkataba na klabu na kwa sababu hiyo wakaomba; 
    “With that said, we would like to request your good office to do the following; Mark Yanga’s agreement with Mr Okwi to at the prerogative of Yanga to terminate without any need of compensation to Mr Okwi,”.
    Kwa mara nyingine katika barua hii, Yanga SC wanaona suluhisho la tatizo lao na mchezaji ni kuvunja Mkataba na wao walipwe- suala la kuadhibiwa kwa mchezaji bado linabaki kwenye mamlaka za soka.
    Yanga SC kama klabu imekwishashitakiwa sana na kukutwa na hatia ya kukiuka mikataba na waajiri wake, wakiwemo makocha na wachezaji. Nikiwa nina akili zangu timamu, mtu wa kwanza kumsikia ameishitaki FIFA klabu hiyo ni Tambwe Leya (sasa marehemu).
    Yanga SC imeendelea kushitakiwa na kukutwa na hatia hadi na wachezaji na makocha wazalendo- lakini haijawahi kufungiwa kwa kuwa hilo silo suluhisho. FIFA inataka klabu na wachezaji ili mpira uchezwe. Imeweka kanuni za adhabu nyepesi, ili kudhibiti mambo yasiyo ya kiungwana kwenye mchezo na si kukomoa.
    FIFA inachukia sana upangwaji matokeo kwenye mchezo na huko ndiko imeweka adhabu kali- haya mengine ya wachezaji kujisajili mara mbili, klabu kutoheshimu mikataba adhabu zake ni za kawaida sana kwenye kanuni.
    Na hili la Okwi, mwisho wa siku litapatiwa ufumbuzi na mchezaji atacheza, lakini kwa ilipofikia si Yanga tena. 
    Suala hili la Okwi lingekuwa jepesi na pengine leo hii lisingekuwa tena mjadala kwenye sika yetu, iwapo TFF ingelishughulikia mapema.
    Yanga SC iliwasilisha barua Juni 27, wakati mzuri tu ambao kama madai yao yangesikilizwa, ina maana hata kama Okwi angeshindwa kesi, angelipa fedha kidogo tu walizoomba Yanga SC.
    Lakini baada ya TFF kuchelewa kutoa majibu, yakaibuka mengine ambayo yakaifanya Yanga SC idai fidia ya dola 200,000.
    Hapo ndipo TFF ikawaandikia barua wote, Yanga na Okwi kuwaita kwenye kikao cha Kamati ya Sheria Maadili na Hadhi za Wachezaji Septemba 6, mwaka huu.
    Baada ya wito huo, Okwi ndipo akaibukia Simba SC akishikilia msimamo Yanga imevunja naye Mkataba na inamdai fidia, hivyo ameomba kipindi ambacho ana kesi nao, acheze Simba SC kulinda kipaji chake.
    Simba SC watampokea hata kwa mdundiko Okwi, lakini mwisho wa siku usajili wake utapitishwa TFF na ili ufike huko, lazima awe amesajiliwa ndani ya muda uliowekwa.
    Ajabu sasa, TFF ilipanga kuwakutanisha Yanga na Okwi katika siku ambayo dirisha la usajili la kimataifa linafungwa, maana yake nini hapa?
    Kwa ujumla, TFF imechangia kwa kiasi kikubwa kuukuza mgogoro wa Yanga na Okwi na sijui ni kwa faida ya nani. Tukijaaliwa Jumapili tena. Alamsiki. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TFF IMEWAFIKISHA HAPA YANGA NA OKWI, KWA FAIDA YA NANI? Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top