ITALIA imeanza vyema kampeni za kufuzu Euro 2016 baada ya kuichapa Norway mabao 2-0 kocha Antonio Conte akiendeleza wimbi la ushindi katika mwanzo wake kazini.
Simon Zaza alifunga bao lake la kwanza timu ya taifa dakika ya 16 katika mchezo ambao pengo la mshambuliaji Mario Balotelli anayetumikia adhabu halikuonekana sana, kabla ya beki wa kati wa Juventus, Leonardo Bonucci alifunga bao la pili dakika ya 62.
Kikosi cha Norway kilikuwa: Nyland, Forren, Nordtveit, Elabdellaoui, Flo, Nielsen/Elyounoussi dk50, Johansen, Skjelbred/Pedersen dk75, Jenssen/Tettey dk70, Daehli na King.
Italy: Buffon, Ranocchia, Bonucci, Astori, Giaccherini, Florenzi/Poli dk87, De Rossi, De Sciglio, Darmian/Pasqual dk61, Immobile na Zaza/Destro dk83.
0 comments:
Post a Comment