MSHAMBULIAJI Danny Welbeck amesema kwamba alikuwa ana ndoto ya kucheza Arsenal hata kabla ya uhamisho wake wa Pauni Milioni 16 kwenda Emirates kutoka Manchester United.
Welbeck amesema hayo katika mahojiano na tovuti ya Arsenal kwamba wakati wote amekuwa akivutiwa mno na staili ya uchezaji ya timu yake mpya na alitamani siku moja kuhamishia huduma zake The Gunners.
Mshambuliaji huyo wa England ameelezea pia namna alivyovutiwa na uhamisho huo katika siku ya mwisho ya kufunga pazia la usajili.
"Ni wakati wa kuvutia kwangu," amesema. "Ni babu kubwa kuwa sehemu ya klabu hii na timu ambayo wakati wote nimekuwa nikiitazama katika Ligi Kuu. Nimekuwa nikipenda kuchezea timu hii kabla. Na hatimaye kufanikisha hili, ni jambo la kuvutuia sana,".

Ndoto zimetimia: Danny Welbeck amesema kucheza Arsenal ni ndoto yake ya siku nyingi


.png)
0 comments:
Post a Comment