• HABARI MPYA

    Wednesday, May 30, 2018

    WACHEZAJI WAPYA WAZUIWA MICHUANO YA SPORTPESA SUPER CUP

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    WAANDAAJI wa michuano ya SportPesa Super Cup inayotarajiwa kuanza nchini Kenya Jumamosi wamezuia wachezaji wapya wanaotaka kusajiliwa kwa msimu ujao kucheza michuano hiyo.
    Bin Zubeiry Sports – Online inafahamu kwamba timu zote zinazokwenda kushiriki michuano hiyo zimekwishaambiwa juu ya kutohusisha wachezaji wapya zinazowasajili kwa sasa.
    Maana yake vikosi vilivyomaliza msimu wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu huu ndivyo vitakavyoshiriki pia michuano ya SportPesa Super Cup. 

    Katika michuano hiyo inayoanzia hatua ya Robo Fainali, Simba SC watafungua dimba na Kariobangi Sharks Juni 3 na Yanga na Kakamega Homeboys Juni 4, mechi zote zikichezwa Uwanja wa Afraha, Nakuru, Gor Mahia itaanza na JKU Juni 3, wakati Singida United itaanza na AFC Leopards Juni 5. 
    Ikumbukwe bingwa wa michuano hiyo ataondoka kitita cha dola za Kimarekani, 30,000, mshindi wa pili dola 10,000, wa tatu dola 7,500 zitakazoishia Nusu Fainali dola 5,000 na za Robo Fainali dola 2,500.
    Pamoja na dola 30,000, bingwa wa michuano hiyo kwa mwaka huu atapata fursa ya kwenda kumenyana na klabu ya Everton nchini England.
    Mwaka jana Gor Mahia ilikuwa bingwa wa kwanza wa michuano hiyo baada ya kuwafunga mahasimu wao, AFC Leopard 2-1 katika fainali kwenye michuano iliyofanyika Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: WACHEZAJI WAPYA WAZUIWA MICHUANO YA SPORTPESA SUPER CUP Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top