• HABARI MPYA

    Tuesday, May 29, 2018

    WACHEZAJI WA AZAM FC WAPEWA MAPUMZIKO HADI JULAI 3

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    WACHEZAJI wa Azam FC, wamepewa mapumziko ya siku 35 hadi Julai 3 mwaka huu watakaporipoti kuanza maandalizi ya msimu ujao.
    Azam FC imefunga msimu jana kwa mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) dhidi ya Yanga, ikiibuka na ushindi wa mabao 3-1 na kujihakikisha kumaliza nafasi ya pili nyuma ya Simba kwa pointi 58.
    Ofisa Habari wa Azam FC, Jaffar Idd, amesema kwamba kwa wachezaji wote watakaosajiliwa na waliopo kikosini hivi sasa wanatakiwa kuripoti Julai 3 kwa ajili ya kuanza mchakamchaka wa maandalizi ya msimu ujao 2018-2019.
    Wachezaji wa Azam FC wamepewa mapumziko hadi Julai 3, mwaka huu  

    “Tutakaporejea tutafanya maandalizi kwa siku kadhaa kabla ya kuelekea nchini Uganda tulipofanya maandalizi ya msimu uliomalizika (pre season) ambapo huko tutacheza mechi kadhaa za kirafiki kama tulivyofanya msimu uliopita kabla ya kurejea nchini,” alisema.
    Azam FC ikiwa nchini Uganda kujiandaa na msimu ulimalizika ilicheza mechi tano za kirafiki, ikitoka sare dhidi ya timu ya Taifa ya Uganda ‘The Cranes’ (2-2), KCCA (1-1), ikazinyuka URA (2-0), Onduparaka (3-0) na Vipers (1-0).
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: WACHEZAJI WA AZAM FC WAPEWA MAPUMZIKO HADI JULAI 3 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top