NAHODHA wa Brazil, Neymar jana alimfanya kocha mpya wa timu hiyo, Carlos Dunga aanze maisha vizuri baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Colombia katika mchezo wa kirafiki Uwanja wa Sun Light mjini Miami.
Neymar alifunga bao hilo pekee dakika ya 83 katika mchezo ambao mshambuliaji mpya wa Manchester United, Radamel Falcao alitokea benchi dakika ya 77 kwenda kuchukua nafasi ya James Rodriquez, lakini hakufurukuta.
Colombia ilimpoteza winga wake Juan Cudrado aliyetolewa kwa kadi nyekundu kipindi cha pili.
Kikosi cha Brazil kilikuwa: Jefferson, Maicon/Elias dk45, Miranda, David Luiz/Marquinhos dk80, Filipe Luis, Ramires/Fernandinho dk45, Luiz Gustavo, Willian/Coutinho dk72, Tardelli/Robinho dk77, Oscar/Everton Ribeiro dk72 na Neymar.
Colombia: Ospina; Zuniga/Mejia dk72, Zapata, Valdes, Armero; Cuadrado, Ramirez/Arias dk45, Sanchez/Ramos dk85, Rodriguez/Falcao dk77, Martinez/Guarin dk64 na Gutierrez/Bacca dk64.
0 comments:
Post a Comment