JUNI 29, Simba SC ilipata uongozi mpya chini ya Rais, Evans Elieza Aveva aliyepita kiulaini baada ya aliyetarajiwa kuwa mpinzani wake mkubwa, Michael Richard Wambura kuenguliwa.
Wambura alienguliwa na Kamati ya Uchaguzi ya klabu kwa kukiuka kanuni za uchaguzi, baada ya kukutwa na hatia ya kufanya kampeni kabla ya muda.
Bahati mbaya zaidi kwake, Wambura amefutwa uanachama baada ya kukutwa na hatia nyingine ya kuipeleka klabu kwenye mahakama za dola, jambo ambalo ni kinyume cha maelekezo ya TFF, CAF na FIFA.
Aveva ameingia madarakani na timu imara yenye Makamu wa Rais, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ na Wajumbe kama Said Tuliy, Iddi Kajuna, Collins Frisch, Ally Suru na wengine.
Lakini kikubwa kuhusu Aveva, inafahamika anatokea kundi la Friends Of Simba lilio chini ya Mwenyekiti, Zacharia Hans Poppe.
Naijua vizuri Friends Of Simba na malengo ya kuundwa kwake- vile vikao vya pale Gogo Hotel akina Jaji Mihayo, Amin Bakhroun (sasa marehemu), Aveva, Crescentius Magori, Jerry Yambi, Mzee Moshi na wengineo, ndiyo chanzo vya ujio wa kikundi imara na gumzo sasa katika soka ya Tanzania, (F.O.S.).
Kufanya vibaya kwa Simba SC kati ya mwaka 1998 na 2000 huku klabu ikiwa dhaifu kiuchumi ndio sababu ya kuundwa Friends.
Friends haikuwa na nia ya moja kwa moja ya wajumbe wake kuingia kuongoza Simba SC, bali kusaidia ustawi wa klabu kuanzia na upatikanaji wa viongozi wa bora na baadaye wafadhili.
Kwa kuwa wengi wao hawakuwa wanachama, F.O.S. ilisaidia kushawishi klabu kupanua wigo wa wanachama kutoka wale 250 hadi 300 na sasa klabu ina maelfu ya wanachama.
Baada ya kuona watu ambao wanaingia madarakani wanashindwa kuifanya Simba SC iwe klabu kubwa Afrika kwa maana halisi, Friends Of Simba wakaamua sasa waichukue wao wenyewe timu.
Na kwa sababu F.O.S. inafahamika juu ya nguvu yake, ikiwa imekwishatoa kiongozi wa juu wa TFF, Magori aliyekuwa Makamu wa Rais, imetoa wabunge, Mawaziri na viongozi katika sekta mbalimbali nchini, haikuwa rahisi kwao kuweka mtu wao madarakani.
F.O.S. ni wapambanaji, wanapotaka jambo lao liwe, linakuwa. Ni watu wa mipango na wenye mshikamano usioyumba.
Awali, walitaka kumsimamisha Mwenyekiti wao, Hans Poppe akapigwa mizengwe, lakini hawakurudi nyuma, wakamteua mtu mwingine, Aveva ambaye sina shaka ni mahiri, shupavu na mweledi mwenye mapenzi ya dhati ya Simba.
F.O.S. inafahamika kama inaundwa na watu wenye uwezo mkubwa wa kifedha, lakini wapo vijana wengine wa kawaida ndani yake na wanapewa heshima yao.
Hizo ni sera za Kassim Dewji, kigogo wa F.O.S. ambaye alianza kuwandaa vijana kama Said Tuliy wakati bado wachanga, ili waje kuwa vigogo wa Simba baadaye.
Lakini nyuma ya yote, ni matarajio ya wanachama wa Simba SC baada ya klabu yao kushikwa na F.O.S.
Imani iliyopo ni kubwa sana, kweli wakati wa kampeni zake Aveva alisema pointi tatu ndio muhimu zaidi, kwake lakini watu wangependa kuiona klabu inabadilika pia chini ya utawala wake.
Simba SC imesajili wachezaji wapya wazuri, akina Pierre Kwizera, Paul Kiongera, Emmanuel Okwi, Elias Maguri wote hawa wangechangia mamilioni ya fedha katika klabu kupitia mauzo ya jezi zenye majina yao.
Tena mambo haya, Friends yapo ndani ya uwezo wao, Kassim Dewji ndiye bingwa wa kusambaza jezi hivi sasa Tanzania ingawa umaarufu wake ulitokana na mgahawa wa Food World, sasa Hadiz.
Hatujasikia kitu kuhusu mradi wa ujenzi wa Uwanja wa Simba SC tangu F.O.S. wafanikiwe kuweka mtu wao madarakani na kwa ujumla kasi yao haiendani na matarajio ya wengi.
Haiwezekani watu wote ndani ya F.O.S. washughulike na timu tu, lazima watu wagawane majukumu na wengine washughulikie masuala mengine ya kimaendeleo katika klabu.
Simba SC inahitaji wadhamini zaidi, inahitaji mikataba zaidi ya kibiashara, tovuti imekufa, yaani Simba SC bado ipo kama ilivokuwa wakati wa Alhaj Ismail Aden Rage.
Friends Of Simba watuonyeshe kama Simba SC sasa imeshikwa na wajanja- klabu haina hata tovuti bwana wakati Hans Popp mmoja tu ana tovuti yake! Tukijaaliwa Jumatano.

0 comments:
Post a Comment