TIMU ya Uswisi imeibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Bosnia & Herzegovina katika mchezo wa Kundi B Fainali za Kombe la Dunia usiku huu Uwanja wa SoFi Stadium, Inglewood, Los Angeles County, California, Marekani
Mabao ya Uswisi yamefungwa na viungo, Johan Manzambi wa Freiburg ya Ujerumani, mzaliwa Geneva kwa wazazi kutoka Angola na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), mawili dakika ya 74 na 90, Rubén Estephan Vargas Martínez wa Sevilla ya Hispania dakika ya 84 na Nahodha, kiungo wa ulinzi, Granit Xhaka wa Sunderland ya England dakika ya 90’+7 kwa penalti.
Bao pekee la ya Bosnia & Herzegovina limefungwa na kiungo wa Slovan Liberec ya Jamhuri ya Czech, Ermin Mahmić dakika ya 90’+3.
Mchezo mwingine wa kundi hilo unaendelea hivi sasa baina ya wenyeji, Canada na Qatar Uwanja wa BC Place, Vancouver nchini Canada.



.png)
0 comments:
Post a Comment