TIMU ya TRA United imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha.
Kiungo Said Ally Mkopi alianza kuifungia Mtibwa Sugar dakika ya pili tu, kabla ya beki wa kushoto Mganda, Christopher Tebandeke kuisawazishia TRA United dakika ya tisa na mshambuliaji Shaaban Iddi Chilunda akafunga la ushindi dakika ya 90.
Kwa matokeo hayo, TRA United inafikisha pointi 37 na kusogea nafasi ya tano, wakati Mtibwa Sugar inabaki na pointi zake 26 katika nafasi ya 10 baada ya timu zote kucheza mechi 24 kwenye ligi ya timu 16.
Ikumbukwe mwisho wa msimu mbili zitashuka Daraja moja kwa moja, wakati nyingine mbili zitakazomaliza nafasi ya 14 na 13 zitamenyana baina yao kwa mechi mbili za nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla atasalia Ligi Kuu.
Timu itakayofungwa itakwenda kumenyana na timu kutoka Ligi ya Championship katika mechi nyingine mbili za mchujo nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla ndiye atacheza Ligi Kuu msimu ujao.



.png)
0 comments:
Post a Comment