• HABARI MPYA

    Wednesday, May 20, 2026

    VERON MOSENGO OMBA RAIS MPYA WA SOKA YA DRC


    ALIYEKUWA Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Véron Mosengo-Omba (66) amechaguliwa kuwa Rais wa Shirikisho la Soka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (FECOFA).
    Akiwa mgombea pekee baada ya wengine kujiuzulu na kuenguliwa, Véron Mosengo amepata kura 60 kati ya 65 zilizopigwa na sasa anachukua nafasi ya Constant Omari, aliyeongoza FECOFA kwa miaka 18 kuanzia mwaka 2003 hadi 2021.
    Mzaliwa huyo wa Kinshasa, Mosengo-Omba mwenye uraia wa Uswisi pia ataiongoza FECOFA kwa miaka minne kwa mujibu wa Katiba kabla ya kuitisha uchaguzi mwingine.
    Veron Mosengo-Omba alijiuzulu Ukatibu Mkuu wa CAF Machi mwaka 30 huu, 2026 kwa shinikizo la kufikia la umri wa kustaafu, miaka 65 baada ya kushika wadhifa huo kuanzia Machi 14, mwaka 2021.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: VERON MOSENGO OMBA RAIS MPYA WA SOKA YA DRC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top