• HABARI MPYA

    Sunday, May 17, 2026

    SIMBA SC YAICHAPA TRA 4-0 NA KUTINGA NUSU FAINALI KOMBE LA CRDB KIBABE


    TIMU ya Simba SC imefanikiwa kwenda Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), michuano inayodhaminiwa na Benki ya CRDB baada ya ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya TRA United usiku wa leo Uwanja wa KMC Complex, Mwenge, Dar es Salaam.
    Mabao ya Simba SC yamefungwa na kiungo Mzambia, Clatous Chotta Chama dakika ya sita, winga Muivory Coast, Alain Anicet Oura dakika ya 26, Suleiman Abdallah Mwalimu dakika ya 64 na kiungo chipukizi, Bashiri Kibaila aliyepandishwa kutoka timu ya vijana dakika ya 78.
    Simba sasa watakutana na Coastal Union katika Nusu Fainali, wakati Azam FC itamenyana na mabingwa watetezi, Yanga katika Nusu Fainali nyingine ya Kombe la CRDB mwezi ujao. 
    Azam FC sasa watakutana na Yanga SC katika Nusu Fainali ya michuano hiyo baada ya mabingwa watetezi kuwatoa JKT Tanzania kwa kuwachapa mabao 2-0 jana Uwanja wa Meja Jenerali Charles Isamuhyo, Mbweni, Dar es Salaam.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA SC YAICHAPA TRA 4-0 NA KUTINGA NUSU FAINALI KOMBE LA CRDB KIBABE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top