TIMU ya Coastal Union imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wenyeji, Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara mchana wa leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
Mabao ya Coastal Union yamefungwa na mshambuliaji Maabad Maulid Maabad dakika ya 35 na kiungo Saad Mwanza dakika ya 74 na kwa ushindi huo Wana Mangush wanafikisha pointi 25 na kuruka hadi nafasi ya 10 kutoka ya 13.
Kwa upande wao Mbeya City baada ya kupoteza mchezo huo nyumbani wanabaki na pointi zao 21 nafasi ya 14 kwenye ligi ya timu 16, ambayo mwisho wa msimu timu mbili zitashuka Daraja.
Timu nyingine mbili zitakazomaliza nafasi ya 14 na 13 zitamenyana baina yao kwa mechi mbili za nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla atasalia Ligi Kuu.
Timu itakayofungwa itakwenda kumenyana na timu kutoka Ligi ya Championship katika mechi nyingine mbili za mchujo nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla ndiye atacheza Ligi Kuu msimu ujao.



.png)
0 comments:
Post a Comment