• HABARI MPYA

    Wednesday, May 20, 2026

    DODOMA JIJI YAAMBULIA SARE KWA MASHUJAA FC, 1-1 JAMHURI


    TIMU ya Dodoma Jiji Fc imelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Mashujaa FC usiku huu katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara uliofanyika Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
    Mshambuliaji Edgar William alianza kuifungia Dodoma Jiji FC dakika ya 11, kabla ya kiungo Balama Mapinduzi ‘Kipenseli’ kuisawazishia Mashujaa FC dakika ya 86.
    Kwa matokeo hayo, Dodoma Jiji inafikisha pointi 33 ingawa inabaki nafasi ya nane, mbele ya Mashujaa FC yenye pointi 27 katika nafasi ya tisa baada ya timu hizo kucheza mechi 24 kwenye ligi ya timu 16.
    Ikumbukwe mwisho wa msimu mbili zitashuka Daraja moja kwa moja, wakati nyingine mbili zitakazomaliza nafasi ya 14 na 13 zitamenyana baina yao kwa mechi mbili za nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla atasalia Ligi Kuu.
    Timu itakayofungwa itakwenda kumenyana na timu kutoka Ligi ya Championship katika mechi nyingine mbili za mchujo nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla ndiye atacheza Ligi Kuu msimu ujao.   

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: DODOMA JIJI YAAMBULIA SARE KWA MASHUJAA FC, 1-1 JAMHURI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top