TIMU ya Singida Black Stars imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Namungo FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Airtel Mwigulu, Singida.
Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, winga wa Kimataifa wa Burundi, Mossi Nduwumwe dakika ya 68 na kwa ushindi huo, Singida Black Stars wanafikisha pointi 38 katika mchezo wa 23 na kurejea nafasi ya nne, wakati Namungo FC inabaki na pointi zake 24 za mechi 23 pia nafasi ya 11 kwenye ligi ya timu 16.
Ikumbukwe mwisho wa msimu timu mbili zitashuka Daraja na mbili zitakazomaliza nafasi ya 14 na 13 zitamenyana baina yao kwa mechi mbili za nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla atasalia Ligi Kuu.
Timu itakayofungwa itakwenda kumenyana na timu kutoka Ligi ya Championship katika mechi nyingine mbili za mchujo nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla ndiye atacheza Ligi Kuu msimu ujao.



.png)
0 comments:
Post a Comment