TIMU ya Azam FC imefanikiwa kwenda Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), michuano inayodhaminiwa na Benki ya CRDB baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wenyeji, Mashujaa FC jioni ya leo Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma.
Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, winga Iddi Suleiman Ally ‘Nado’ dakika ya 45’+4 kwa shuti la mpira wa adhabu lililompita kipa wa zamani wa Yanga, Erick Johola.
Azam FC sasa watakutana na Yanga SC katika Nusu Fainali ya michuano hiyo baada ya mabingwa watetezi kuwatoa JKT Tanzania kwa kuwachapa mabao 2-0 jana Uwanja wa Meja Jenerali Charles Isamuhyo, Mbweni, Dar es Salaam.



.png)
0 comments:
Post a Comment