• HABARI MPYA

    Friday, May 15, 2026

    SERENGETI BOYS YAANZA VYEMA AFCON U17, YAICHAPA MSUMBIJI 3-0 MOROCCO


    TIMU ya Tanzania jana ilianza vyema Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 (AFCON U17) baada ya ushindi wa mabao 3–0 dhidi ya Msumbiji katika mchezo wa Kundi C uliofanyika Pitch 11 ya Uwanja wa Mohammed VI Football Academy Jijini Salé Kaskazini-Magharibi mwa  Morocco.
    Mabao ya Serengeti Boys yalifungwa na Dismas Athanas Shida dakika ya 26, Paschal Miambo aliyejifunga dakika ya 35 na Razaki Mbegelendi dakika ya 63.
    Mechi nyingine ya kundi hilo jana Mali ilitoka suluhu (0–0) na Angola Pitch 3 ya Uwanja huo huo wa Mohammed VI Football Academy, Salé.
    Serengeti Boys itashuka tena dimbani Jumapili, Mei 17 kumenya na Angola kabla ya kukamilisha mechi zake za kundi C kwa kumenyana na Mali Jumatano, Mei 20.
    Ikumbukwe Tanzania inashiriki Fainali za U17 kwa mara ya tatu baada ya mwaka 2017 nchini Gabon na 2019 Mumbai, Tanzania ambako mara zote walitolewa katika hatua ya makundi.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SERENGETI BOYS YAANZA VYEMA AFCON U17, YAICHAPA MSUMBIJI 3-0 MOROCCO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top