TIMU ya Fountain Gate imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya TRA United katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha.
Mabao yote ya Fountain Gate yamefungwa na kiungo Ismail Aziz Kader dakika ya 44 na 45’+2 baada ya wenyeji, TRA United kutangulia kwa bao la beki wake wa kulia Mnigeria, John Lazarus dakika ya 35.
Kwa ushindi huo, Fountain Gate inafikisha pointi 29 na kusogea nafasi ya tisa kutoka ya 11, wakati TRA United wanabaki na pointi zao 37 nafasi ya sita baada ya timu hizo zote kucheza mechi 25 kwenye ligi hiyo ya timu 16.
Ikumbukwe mwisho wa msimu timu mbili zitashuka Daraja moja kwa moja, wakati nyingine mbili zitakazomaliza nafasi ya 14 na 13 zitamenyana baina yao kwa mechi mbili za nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla atasalia Ligi Kuu.
Timu itakayofungwa itakwenda kumenyana na timu kutoka Ligi ya Championship katika mechi nyingine mbili za mchujo nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla ndiye atacheza Ligi Kuu msimu ujao.



.png)
0 comments:
Post a Comment