• HABARI MPYA

    Tuesday, May 12, 2026

    TRA UNITED YAAMBULIA SARE KWA JKT TANZANIA, 1-1 ARUSHA


    WENYEJI, TRA United wamelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na JKT Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha.
    Mshambuliaji Mganda, Joseph Akandwanaho alianza kuifungia TRA United dakika ya 20, kabla ya beki wa kulia, Salum Khamis Salum ‘Gado kuisawazishia JKT Tanzania dakika 10 baadaye.
    Kwa matokeo hayo, TRA United inafikisha pointi 34, ingawa inabaki nafasi ya sita ikiendelea kuzidiwa pointi mbili na JKT Tanzania inayoshika nafasi ya tano baada ya timu hizo zote kucheza mechi 23. 

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TRA UNITED YAAMBULIA SARE KWA JKT TANZANIA, 1-1 ARUSHA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top