MABINGWA watetezi, Yanga SC wamefanikiwa kutinga Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), michuano inayodhaminiwa na Benki ya CRDB baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wenyeji, JKT Tanzania usiku huu Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Mbweni, Dar es Salaam.
Beki Hassan Wahabi alijifunga dakika ya 33 akijaribu kuokoa krosi fupi ya beki Mkongo, Chadrack Issaka Boka kuipatia Yanga SC bao la kwanza, kabla ya kiungo Mudathir Yahya Abbas kufunga bao la pili dakika ya 40.
Mabao yote ya Yanga leo yalitokana na kazi nzuri ya kiungo Muivory Coast, Peodoh Pacome Zouzoua ambaye leo alikuwa katika kiwango kizuri baada ya kuyumba kwenye mechi kadhaa zilizopita.
Yanga inakuwa na timu ya pili kwenda Nusu Fainali ya Kombe la CRDB baada ya Coastal Union ambayo jioni ya leo ilitoa Singida Black Stars kwa Penalti 4-2 kufuatia sare ya bila mabao ndani ya dakika 90 Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga.



.png)
0 comments:
Post a Comment