Klabu ya Black Leopard ya Afrika Kusini, iliyokuwa ifike jana
nchini sasa inatarajiwa kufika leo, tayari kwa mchezo wa kirafiki dhidi ya
mabingwa wa Afrika Mashariki na Kati, Yanga SC kesho Uwanja wa Taifa mjini Dar
es Salaam. Taarifa hiyo ni kwa mujibu wa waratibu wa mechi hiyo, kampuni ya
Prime Time Promotions ya Dar es Salaam. Pichani ni kipa namba wa timu hiyo, Mganda, Posnet Omony akiwa katika moja ya mechi za klabu hiyo 'tishio' katika Ligi ya Afrika Kusini.
|