• HABARI MPYA

  Alhamisi, Januari 24, 2013

  SIMBA YAPIGWA 1-0 NA LEOPARD TAIFA

  Mshambuliaji wa Simba SC, Ramadhan Singano ‘Messi’, 
  kushoto akijaribu kumtoka beki wa Black Leopard ya 
  Afrika Kusini, Vencent Mabusera jioni hii Uwanja wa
   Taifa, Dar es Salaam katika mchezo wa kirafiki.
   Picha na Jackson Odoyo wa habarimpya.com.

  Na Princess Asia
  IKICHEZESHA wachezaji wake vijana wanaoinukia vema, Simba SC jioni hii imelala 1-0 mbele ya Black Leopard ya Afrika Kusini katika mchezo wa kirafiki uliofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Bao pekee la washindi katika mchezo huo, lilifungwa na beki Hassan Isihaka aliyejifunga katika harakati za kuokoa dakika ya saba tu ya mchezo huo.
  Pamoja na kufungwa, watoto hao wa Simba SC waliokwenda ziara ya wiki mbili Oman, walicheza soka maridadi na kuwaburudisha wapenzi wa timu hiyo.
  Ushindi huo, unaitoa mrithi Leopard ambayo awali katika ziara yake ya wiki moja nchini ilifungwa mechi mbili na Yanga SC, 3-2 Dar es Salaam Jumamosi na 2-1 jana CCM Kirumba, Mwanza.
  Katika mchezo huo, kikosi cha Simba kilikuwa; Abuu Hashim, William Weta, Emiry Mgeta, Hassan Isihaka, Hassan Hatibu, Said Ndemla, Ramadhani Singano, Ibrahim Ajid/Haruna Shamte, Marid Kaheza, Rashid Ismail na Miraji Madenge.
  Leopard; Azwindn Maphala, Ermort Azaga, Thulan Ntishgila, Humphey Khoza, Vicent Mabusela, Tiyana Mabunda, Mongezi Bobe, Mahlatse Maake, Michael Nkambula , Mxolis Ngunede na Kodney Ramagalela.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: SIMBA YAPIGWA 1-0 NA LEOPARD TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top