• HABARI MPYA

  Jumanne, Januari 29, 2013

  KABANGE TWITE KUSUBIRI MSIMU UJAO YANGA

  Kabange

  Na Boniface Wambura
  KIUNGO Alain Kabange Twite hataweza kuichezea Yanga msimu huu (2012/2013) baada ya klabu hiyo kuingiza nyaraka zenye upungufu wakati ikimuombea Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kwa njia ya mtandao (Transfer Matching System- TMS).
  Kwa mujibu wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), baadhi ya nyaraka zenye upungufu katika maombi hayo ni mkataba kati ya Twite na Yanga, lakini vile vile makubaliano ya mkopo (Loan Agreement) kati ya Yanga na FC Lupopo ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) ambayo ndiyo inayommiliki mchezaji huyo.
  Ili mchezaji aweze kupata ITC kwa njia ya TMS, kwa mujibu wa Kanuni za Uhamisho wa Wachezaji za TFF kuna nyaraka kadhaa muhimu zinatakiwa kukamilika katika maombi hayo ili hati hiyo iweze kupatikana.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: KABANGE TWITE KUSUBIRI MSIMU UJAO YANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top