• HABARI MPYA

    Thursday, January 24, 2013

    SIMBA HUENDA IKAAMBULIA DOLA 200,000 TU MAUZO YA OKWI

    Okwi

    Na Mahmoud Zubeiry
    PAMOJA na kumuuza kwa dau la dola za Kimarekani, 300,000 mshambuliaji wake wa kimataifa wa Uganda, Emannuel Okwi katika klabu ya Etoile du Sahel ya Tunisia, lakini klabu hiyo inaweza kujikuta inaambulia dola 200,000 tu.
    Hiyo inatokana na makato mengine ya kisheria yanayoingia katika mauzo hayo, ikiwemo asilimia 20 ya klabu yake ya zamani, SC Villa ya Uganda, ambayo ni sawa na dola 60,000.
    Pamoja na hayo, inaelezwa kuna fungu la wakala aliyefanikisha mpango huyo ambaye ana mkataba na Okwi.
    Simba ilimuuza Okwi klabu ya Etoile du Sahel ya Tunisia kwa dau la dola za Kimarekani 300,000, zaidi ya Sh Milioni 450 za Tanzania.
    Okwi, aliyezaliwa Desemba 25, mwaka 1992 aliisajiliwa Simba akitoea SC Villa ya Uganda mwaka 2010 akiwa kinda wa miaka 17, akisajiliwa kwa dau la dola za Kimarekani 40,000.
    Baada ya kumaliza mkataba wake wa awali, Desemba mwaka jana aliongeza mkataba wa miaka miwili na Simba SC ambao kabla hajaanza kuutumikia, anahamia Sahel.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: SIMBA HUENDA IKAAMBULIA DOLA 200,000 TU MAUZO YA OKWI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top