• HABARI MPYA

  Jumatatu, Januari 28, 2013

  BABU WA SIMBA 'HATUMI MTOTO DUKANI' MWANZO MWISHO

  Tofauti na makocha wengi wa Kizungu wanaokuja nchini kufanya kazi, katika mechi huwaachia Wasaidizi wao wazalendo majukumu ya kuzungumza na wachezaji mchezo unapoendelea, kocha wa Simba, Mfaransa Patrick Liewig juzi katika mechi dhidi ya African Lyon alikuwa akipigizana nao mwenyewe kelele, hadi kuna wakati mwamuzi wa akiba alisimama kumuamuru aketi kidogo baada ya kusimama muda mrefu mfululizo akisema nao.

  Babu Liewig anasema nao

  Babu anasema nao wakati wasaidizi wake wanakula kipupwe kwenye sofa

  Hapa refa anakuja kumuambia akae 

  Hapa Julio aliinuka kumsaidia kusema nao

  Refa anamuacha Julio asimame, anamuambia Babu akakae

  Babu anauliza, mbona Julio humuambii akae, refa anamuambia huyu kasimama sasa hivi, we tangu maechi ianze bwana hadi sasa hivi mnaongoza 3-1 bado hujakaa tu

  Babu kakubali yaishe anakaa

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: BABU WA SIMBA 'HATUMI MTOTO DUKANI' MWANZO MWISHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top