• HABARI MPYA

    Saturday, January 26, 2013

    SIMBA SC ILIVYOUA KWA SUMU ZA OMAN LEO, HUYO NGASSA BALAA NA KASEJA BADO WAMO, KUNA CHANONGO USIMPIMIE

    Mshambuliaji wa Simba SC, Mrisho Ngassa kulia akipongezwa na wenzake baada ya kufunga jioni hii katika ushindi wa 3-1 dhidi ya African Lyon katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, uliofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Ngassa alifunga mabao mawili.

    Ngassa akishangilia na Haruna Moshi 'Boban kwenye benchi', huku wachezaji wengine wakimtazama kwa shauku

    Beki wa Simba SC, Mussa Mudde akimdhibiti mshambuliaji wa Lyon

    Juma Kaseja amepangua penalti ya Shamte Ally 

    Beki wa Lyon, Job Ibrahim akikimbilia mpira dhidi ya kiungo wa Simba SC, Ramadhani Chombo 'Redondo'

    Job Ibrahim akijaribu kumkimbiza kiungo wa Simba SC, Amri Kiemba kulia

    Job akiwa amelala kuondosha mpira miguuni mwa Ngassa

    Haruna Chanongo akiruka kwanja la beki wa Lyon na kufanikiwa kupiga krosi iliyounganishwa nyavuni na Ngassa kuwa bao la tatu

    Mabeki wa Lyon wakimdhibiti kiungo wa Simba SC, Amri Kiemba

    Kiemba akipambana na mabeki wa Lyon 

    Ngassa akimtoka Job Ibrahim kufunga bao la pili leo 

    Redondo akifunga bao la kwanza

    Haruna Chanongo akipasua msitu wa mabeki wa Lyon

    Job akiwa amepitia mpira miguuni mwa Ngassa

    Redondo akimshukuru Ngassa kwa pasi ya bao la kwanza la Simba

    Mwinyi Kazimoto akichuana na kiungo wa Lyon

    Kikosi cha Lyon leo
    Kikosi cha Simba SC leo


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: SIMBA SC ILIVYOUA KWA SUMU ZA OMAN LEO, HUYO NGASSA BALAA NA KASEJA BADO WAMO, KUNA CHANONGO USIMPIMIE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top