• HABARI MPYA

    Tuesday, July 19, 2016

    MBEYA CITY YAIFUATA MTIBWA MORO KWA MCHEZO WA KIRAFIKI

    Na Mwandishi Wetu, MBEYA
    SIKU kadhaa baada ya kuanza kwa kambi ya mazoezi kwa ajili ya matayarisho ya msimu mpya tayari  imethibitishwa kuwa kikosi  cha Mbeya City FC kitasafiri hadi mkoani Morogoro kwa ajili ya mchezo wa kujipima nguvu dhidi ya wenyeji Mtibwa Sugar kwenye uwanja wa Jamhuri Julai 30, mwaka huu.
    Kwa mujibu wa kiongozi wa Kanisa la Faith Baptist, Mchungaji  Jerry Wyatt ambaye ndiye mwandaaji na msimamizi mkuu wa mchezo huo, maandalizi yote ya mechi hiyo ya kirafiki itakayoambatana na tamasha kubwa la mahubiri ya neno la Mungu tayari yamekamilika ikiwa ni pamoja na timu zote kuthibitisha kuhudhuria.
    Mtibwa Sugar watacheza na Mbeya City Julai 30 Uwanja wa Jamhuri, Morogoro
    “Maandalizi yote yamekamilika, timu zote zimethibitisha kushiriki katika mchezo huo ambao  utaambana na mahubiri ya neno la Mungu kwenye uwanja wa Jamhuri, naomba watu wajitokeze kwa wingi kuja kushuhudia mchezo mzuri wa kirafiki kutoka kwa timu hizi mbili pia kupata mahubiri mazuri ya neno la Mungu sambamba na matukio mengine mengi” alisema.
    Akiendelea  zaidi Mch Jerry  alisema kuwa kwenye tamasha hilo la neno la Mungu na mchezo wa kirafiki wa soka hakutakuwa na kiingilio chochote kwa watakaofika kwenye uwanja wa Jamhuri na kwa wale watakaopata nafasi wanakaribishwa kuhudhuria ibada kwenye kanisa la Faith Baptist lililopo Kola B siku jumapili ya julai 31.
    “Hakutakuwa na kiingilio, pia wale watakaopata nafasi nawakaribisha  kuhudhuria ibada kwenye kanisa letu  siku ya Jumapili siku ambayo  pia  tutatoa zawadi mbalimbali kwa timu za soka zaidi ya 40 za mjini hapa (Morogoro) kwa maana hiyo litakuwa jambo jema watu wote wakihudhuria”
    Hii ni mara ya pili kwa Mtibwa na City kucheza mchezo wa kirafiki ulioandaliwa na Kanisa  hilo  awali ikiwa ni msimu uliopia ambapo timu hiyo kutoka Manungu iliibuka na ushindai wa bao 1-0 lililofungwa kipindi cha pili na Mohamed  Ibrahim
    City  inatarajia  kuondoka  Mbeya  Julai  28 tayari  kwa mchezo huo  uliopangwa kupigwa  siku jumamosi ya mwisho wa mwezi huo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MBEYA CITY YAIFUATA MTIBWA MORO KWA MCHEZO WA KIRAFIKI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top