• HABARI MPYA

    Friday, July 29, 2016

    MAKONDA KUZINDUA AIRTEL RISING STARS KESHO KARUME

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kesho Jumamosi Julai 30, 2016 anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa mashindano ya kuibua na kukuza vipaji vya wanasoka chipukizi, Airtel Rising Stars Uwanja wa Karume, Ilala mjini Dar es Salaam.
    Sambamba na Makonda, Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi naye amethibitisha kuwako kwenye hafla hiyo ambayo mchezo wa kwanza utazikutanisha timu za Ilala Boys dhidi ya Bombom Ilala, Dar es Salaam. Inawakilishwa na mikoa yote mitatu kisoka ambayo ni Ilala, Kinondoni na Temeke kwa pande zote mbili za wavulana na wasichana.

    Kadhalika, wakuu wa mikoa mingine ambayo mashindano hayo yatafanyika nao watakuwa wageni rasmi katika mikoa yao ambayo ni Mbeya, Mwanza na Morogoro kwa upande wa wavulana pia Arusha, Lindi na Zanzibar kwa upande wa wasichana.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAKONDA KUZINDUA AIRTEL RISING STARS KESHO KARUME Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top