• HABARI MPYA

    Tuesday, July 26, 2016

    YANGA NI YA KUJIPIGIA TU, INAPIGWA TU...NA LEO IMEPIGWA 3-1

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    YANGA SC imeendelea kuboronga katika mechi za Kundi A Kombe la Shirikisho Afrika baada ya jioni ya leo kufungwa mabao 3-1 na wenyeji Medeama FC Uwanja wa Essipong Sports mjini Sekondi-Takoradi, Ghana.
    Huo unakuwa mchezo wa nne mfululizo Yanga inacheza bila kushinda, ikifungwa mara tatu na kutoa sare moja. Yanga ilianza kwa kufungwa na 1-0 na Mo Bejaia nchini Algeria kabla ya kufungwa tena 1-0 na TP Mazembe na kutoka sare ya 1-1 na Medeama mjini Dar es Salaam kabla ya kipigo cha leo.
    Mabao ya Medeama yalifungwa na Daniel Amoah dakika ya saba aliyemalizia kona ya Enock Atta Agyei na Abbas Mohammed mawili dakika ya 23 na 37, wakati la Yanga lilifungwa na Simon Msuva dakika ya 25 kwa penalti baada ya Obrey Chirwa kuangushwa kwenye boksi. Na Yanga ingepigwa 4-1 kama si kipa Deo Munishi ‘Dida’ kupangua mkwaju wa penalti  Malik Akowuah dakika ya 10.
    Matokeo hayo yanamaanisha Yanga inaondoka kwenye mbio za kuwania Nusu Fainali na sasa inacheza kukamilisha ratiba. Mazembe inaendelea kuongoza Kundi A kwa pointi zake saba, ikifuatiwa na MO Bejaia na Medeama ambazo zote kila moja ina popinti tano, wakati Yanga ina pointi moja. Mazembe watakuwa wenyeji wa Bejaia kesho Lubumbashi wakihitimisha raundi za nne. 
    Kikosi cha Yanga kilikuwa; Deo Munishi ‘Dida’, Kevin Yondani/Andrew Vincent dk46, M. Twite, O. Joshua, J. Abdul/Amissi Tambwe dk73, N. Haroub, H. Niyonzima/Juma mahadhi dk46, T. Kamusoko, D. Ngoma, S. Msuva na O. Chirwa.
    Medeama; Daniel Yaw Agyei, Paul Aidoo, Samjuel Adade, Moses Amponsah Sarpong, Daniel Amoah, Malik Akowuah, Kwesi Donsu, Enock Atta Agyei, Eric Kwakwa/ Kwame Boahene dk72, Abbas Mohammed/ Bismark Oppong dk53 na Benard Ofori.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA NI YA KUJIPIGIA TU, INAPIGWA TU...NA LEO IMEPIGWA 3-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top