• HABARI MPYA

    Tuesday, May 13, 2014

    SPURS YAMTUPIA VIRAGO KOCHA SHERWOOD

    KOCHA Tim Sherwood amefukuzwa Tottenham Hotspur kiasi cha miezi sita tang aanze kazi White Hart Lane.
    Sherwood alirithi mikoba ya Andre Villas-Boas Desemba kwa Mkataba wa miezi 18, lakini ameshindwa kuingia katika msimu wa pili na klabu hiyo.
    Nje: Tim Sherwood amefukuzwa Tottenham baada ya miezi sitaOut the door: Levy (centre) has decided to trigger a break clause in Sherwood's contract
    Nje ya mlango: Levy (katikati) ameamua kumtema Sherwood

    Tetesi za kuondolewa kwa Sherwood zilianza mwezi uliopita, na hatimaye Mwenyekiti Daniel Levy kutafuta mtu mwingine mwafaka zaidi.
    Sherwood ameshinda mechi 14 kati ya 28 akiwa kazini, akitoa safe nne na kufungwa 10, Spurs ikimaliza katika nafasi ya sita kwenye msimamo wa ligi, ikizidiwa pointi 10 na Arsenal iliyomaliza nafasi ya nne.
    Mwalimu huyo mwenye umri wa miaka 45 anaweza kupewa ofa mara moja kurejea kurejea klabu ya Daraja la kwanza, Brighton baada ya Oscar Garcia kujiuzulu baada ya kufungwa katika mechi ya Nusu Fainali ya mchujo dhidi ya Derby
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SPURS YAMTUPIA VIRAGO KOCHA SHERWOOD Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top