MSHAMBULIAJI Romelu Lukaku atatolewa chambo kwenda Atletico Madrid ili Chelsea impate Diego Costa.
Lakini inafahamika Mbelgiji huyo itabidi abadilishe msimamo wa kutokwenda kucheza Hispania kwa sababu ya hill kibaguzi baada ya adhabu nyepesi waliyopewa Villarreal kwa kumtupia ndizi Daniel Alves.
Costa ni chaguo kuu la Jose Mourinho katika uhamisho wa usajili ujao na mocha huyo wa Chelsea anataka biashara hiyo ikamilike mapema.
Mlengwa: Chelsea imeanza mazungumzo na Atletico Madrid juu ya mshambuliaji Diego Costa (kulia)
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25, ambaye anatarajiwa kuwamo katika kikosi cha Hispania kitakachoshiriki Fainali za Kombe la Dunia, amefunga mabao 27 msimu huu ana thamani ya Pauni Milioni 32.
Chelsea inafanya maarifa ya kumpata nyota huyo na imekubali kumtoa Lukaku ili wabadlishane.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 21, alitua Stamford Bridge kwa day la Pauni Milioni 18 kutoka Anderlecht mwaka 2011, na amefunga mabao 16 katika mkopo wake Everton msimu huu na anaonekana hana nafasi Chelsea.
Aliingia kwenye vita ya maneno na Mourinho mwishoni mea mwaka jana juu ya uhamisho wake wa muda katika klabu hiyo.
Lukaku alisema yalikuwa ni mawazo ya kocha, wakati Mreno huyo alipingana nays. Lukaku kisha akasema angependa kubaki Everton kwa msimu mwingine, lakini Mourinho alijibu kwa kusema yeye ndiye ataamua mustakabali wa mchezaji huyo.
Lakini licha ya Atletico kuwa jatika nafasi ya kutwaa taji la La Liga na Ligi ya Mabingwa ambako wametinga fainali, kuendelea kwa matukio ya kibaguzi Hispania kunaweza kumfanya Lukaku akatae kwenda kucheza huko.
Villarreal ilipigwa faini ya Pauni 10,000 baada ya shabiki wake kumrushia ndizi beki wa pembeni wa Barcelona, Alves, ambaye baadaye alijibu mapigo kwa kuposti picha kwenye intaneti akilila tunda hilo.
Adhabu nyepesi: Villarreal ilipigwa faini ya Pauni 10,000 tu baada ya shabiki wake kumtupia ndizi Alves uwanjan



.png)
0 comments:
Post a Comment