// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MALINZI AMPA ULAJI MVELLA TFF - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MALINZI AMPA ULAJI MVELLA TFF - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Wednesday, May 21, 2014

    MALINZI AMPA ULAJI MVELLA TFF

    Na Boniface Wambura, Dar es Salaam
    ALIYEKUWA Katibu Mkuu wa Chama cha Soka Iringa (IRFA), Eliud Mvella amejiunga na Sekretarieti ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), chini ya rais wake, Jamal Malinzi.
    Amejiunga na Sekretarieti ya TFF katika Idara ya Sheria na Vyama Wanachama kuanzia leo (Mei 21 mwaka huu) ambapo atashughulikia masuala ya wanachama.
    Mvella alijiuzulu rasmi wadhifa wake IRFA jana (Mei 20 mwaka huu). Mwenyekiti wa IRFA, Cyprian Kwihyava amepokea barua ya kujiuzulu huko ambapo ameelezea masikitiko yake kwa uamuzi huo wa Mvella.
    Rais wa TFF, Jamal Malinzi

    Ni imani ya TFF kuwa Mvella atatumia uzoefu wake wa muda mrefu katika uongozi wa mpira wa miguu kuhakikisha TFF inaimarisha uhusiano wake na wanachama wake.
    TFF ina wanachama 44 ambao ni vyama vya mpira wa miguu vya mikoa, vyama shiriki na klabu za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL).

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MALINZI AMPA ULAJI MVELLA TFF Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top