• HABARI MPYA

    Thursday, May 22, 2014

    WAMBURA, AVEVA NA WAGOMBEA WENGINE KIBAO WAWEKEWA PINGAMIZI KUGOMBEA SIMBA SC

    Na Nagma Khalid, DAR ES SALAAM
    WAGOMBEA wote wa nafasi za Urais kuwekewa pingamizi kuelekea Uchaguzi Mkuu wa klabu ya Simba uliopangwa kufanyika June 29, mwaka huu.
    Wagombea hao wanaochuana kwenye nafasi ya Urais ni Michael Wambura, Evans Aveva na  Andrew Tupa wamekewa pingamizi na wanachama mbalimbali.
    Akizungumza na BIN ZUBEIRY leo, Katibu wa Kamati ya Uchaguzi, Khalid Kamguna alithibitisha kupokea pingamizi za wagombea wote.
    Michael Wambura amewekewa pingamizi sambamba na mpinzani wake, Evans Aveva pichani chini

    “Wagombea wote wamemewekewa pingamizi ila sipotayari kuwataja wale walioweka pingamizi hizo,”alisema
    Licha ya Kamguna kugoma kuwataja walioweka pingamizi, Wambura aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Soka Tanzania(FAT) sasa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) amewekewa pingamizi na mwanachama Swalehe Madijaba mwenye kadi namba 00574 kutoka tawi la Arusha Mjini.
    Mara baada ya kuweka pingamizi hilo, Madijaba alisema ameamua kumuwekea Wambura pingamizi kwa kitendo chake cha kuanza kampeni mapema.
    “Nina ushaidi wa hili ninalosema Wambura ameanza kampeni mapema na katiba yetu ya Simba hairuhusu hivyo ndio mana nimemuwekea pingamizi”alisema.
    Alisema mbali na pingamizi hilo la Wambura amewawawekea pingamizi wagombea wote wa kamati ya utendaji waliopo madarakani kwa sasa.
    Aliwataja wagombea hao ni Ibrahim Masoud, Damian Manembe, Said Pamba, Swed Nkwambi, na Joseph Itang’are ‘Mzee Kinesi’.
    “Hawa wagombea hawajafanya kitu katika kipindi cha miaka minne iliyopita sasa wanataka kurudi madarakani kufanya nini,”Alisema.
    Alisema pingamizi la mwisho alilowasilisha kwenye kamati ya uchaguzi chini ya Katibu Kamguna ni la mgombea Chano Karaha
    “Huyu mgombea tutaona nae tu kwenye usikilizwaji wa pingamizi hivyo siwezi kusema kwanini nimemuwekea kwa sasa,”alisema.
    Naye Kocha wa msaidizi wa zamani wa timu hiyo, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ amewawekea pingamizi na Wajumbe wa Kamati ya utendaji wote waliopo madarakani kwa kukiuka katiba ya timu hiyo.
    “Wao wakimwanga mboga mimi nimemwaga ugali, wale wote ambao walihusika katika kikao kile kilichoniengua nimewawekea pingamizi,”alisema.
    Mbali na Julio, Mwanachama na mchezaji wa zamani wa klabu hiyo, Athur Mwambene amejitosa kumuweka pingamizi mgombea wa nafasi ya Makamu wa Rais Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ na Swedi Mkwabi.
    “Nimemuweka pingamizi Kaburu kwa sababu alijiuzulu na katiba ya Simba inasema ukiwa umejiuzulu unatakiwa ukae miaka mtatu bila kugombea kwa nini achukue fomu,”alisema.
    Wakati Mwambeni akimuwekea pingamizi Kaburu na Swedi, Mwanachama Lucus Mbapila wenye kadi namba 4585 kutoka tawi la Mdomo wa Simba Mwananyamala amemuwekea pingamizi mgombea wa makamu wa rais Swedi Mkwabi kwa kosa la kukiuka kanuni za uchaguzi.
    Pingamizi la mwisho ni la Mwanachama wa Mwinyi Sharrifu Dossi mwenye kadi namba 564 aliyesindikizwa na Chano Almasi aliwawekea pingamizi wajumbe wote wa  Kamati ya utendaji waliomaliza muda wao.
    Pingamizi zote zinatarajiwa kusikilizwa Mei 25 na kamati ya uchaguzi chini ya Mwenyekiti wake Damas Ndumbalo ambapo wagombea na wawekwa pingamizi watahitajika wakati wa kusikilizwa.
    Uchaguzi Mkuu wa timu hiyo unatarajiwa kufanyika  June 29 mwaka huu katika bwalo la Polisi Oysterbay.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: WAMBURA, AVEVA NA WAGOMBEA WENGINE KIBAO WAWEKEWA PINGAMIZI KUGOMBEA SIMBA SC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top