• HABARI MPYA

    Tuesday, May 27, 2014

    VAN GAAL AIFUMUA LISTI YA USAJILI MAN UNITED NA KUWAPIGA CHINI FABREGAS, KROOS...ATAKA WAHOLANZI KIBAO NA SCHWEINSTEIGER

    KOCHA mpya wa Manchester United, Louis van Gaal amewaondoa Cesc Fabregas na Toni Kroos katika orodha ya wachezaji anaotaka kuwasajii msimu ujao na kuelekeza nguvu zake kwa wachezaji wengine  akiwemo mpachika mabao wa Bayern Munich, Bastian Schweinsteiger.
    Mholanzi huyo amesema kwamba, ana matumaini kocha wa Munich, Pep Guardiola atakuwa tayari kusikiliza ofa ya Pauni Milioni 10 kwa ajili ya kiungo huyo mwenye umri wa miaka 29.
    Schweinsteiger, ambaye jina lake lilitajwa pia wakati wa David Moyes akiwa kazini United, pia ana nia ya kwenda kukabiliana na changamoto mpya.
    Ana mipango yake mwenyewe: Louis van Gaal amewatambulisha wachezaji kadhaa wa kusajiliwa atakapoanza kazi
    On the hunt: Bastian Schweinsteiger could be available for £10m and Van Gaal is interested in the midfielder
    Anamuhitaji: Bastian Schweinsteiger anaweza kupatikana kwa dau la Pauni Milioni 10 na Van Gaal anamuhitaji kiungo huyo

    Pia Van Gaal anawataka beki wa kulia wa Feyenoord, Daryl Janmaat, beki wa kati Bruno Martins Indi na beki wa Ajax, Daley Blind na mpango wa kumsajili Kevin Strootman wa AS Roma bado upo, mara itakapothibitika anaweza kupona maumivu yake goti.
    Wakati huo huo, Danny Welbeck amesema amevurugwa kwa kukosa nafasi katika kikosi cha kwanza cha United msimu uliopita, kwani mshambuliaji huyo wa England anataka kupangwa katikati athibitishe uwezo wake wa kufunga kwa kiwango cha juu katika klabu na timu ya taifa. 
    Welbeck amefunga mabao manane katika mechi 21 za timu ya taifa, lakini alikuwa akisotea namba kikosi cha kwanza chini ya David Moyes United. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: VAN GAAL AIFUMUA LISTI YA USAJILI MAN UNITED NA KUWAPIGA CHINI FABREGAS, KROOS...ATAKA WAHOLANZI KIBAO NA SCHWEINSTEIGER Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top