// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); LUIS SUAREZ APASULIWA GOTI, YAELEZWA ATAPONA MAPEMA NA KUWAHI KOMBE LA DUNIA BADO BICHI KUANZIA MECHI NA ENGLAND - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE LUIS SUAREZ APASULIWA GOTI, YAELEZWA ATAPONA MAPEMA NA KUWAHI KOMBE LA DUNIA BADO BICHI KUANZIA MECHI NA ENGLAND - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Thursday, May 22, 2014

    LUIS SUAREZ APASULIWA GOTI, YAELEZWA ATAPONA MAPEMA NA KUWAHI KOMBE LA DUNIA BADO BICHI KUANZIA MECHI NA ENGLAND

    RATIBA YA URUGUAY

    Juni 14: Vs Costa Rica, Saa 2:00 Usiku, Uwanja wa Castelao
    Juni 19: Vs England, Saa 2:00 Usiku, Uwanja wa Sao Paulo
    Juni 24: Vs Italia, Saa 11:00 Jioni, Uwanja wa Das Dunas
    MSHAMBULIAJI Luis Suarez amefanyiwa upasuaji wa goti  na anatarajiwa kupona ndani ya muds na kucheza Fainali za Kombe la Duni, amesema mama yake. 
    Sandra Diaz amesema upasuaji umefanyika kwa mafanikio na mwanawe anatarajiwa kupona ndani ya wiki tatu, ambayo inamaanisha atauwahi mchezo dhidi ya England Juni 19, mwaka huu.  
    Mambo yameenda vizuri: Luis Suarez amefanyiwa upasuaji leo na anaweza kuziwahi Fainali za Kombe la Dunia kuanzia mchezo dhidi ya England

    "Upasuaji umemalizika na tunamshukuru Mungu kila kitu kimekwenda vizuri. Matatizo yaliyokuwa yanamsumbua Luis hayakuwa makubwa sana ," alisema kuzungumzia majeruhi ya mwanawe.
    Uruguay, ambayo imedai Suarez alipata maumivu hayo katika mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu ya England msimu huu, bado inajiamini atacheza Juni 19
    BIN ZUBEIRY inafahamu kwamba maofisa wa soka wa nchi hiyo wanaamini mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27 anaweza kuwa fiti hata wakati wa mchezo wa ufunguzi dhidi ya Costa Rica, lakini ataanza kucheza siku tano baadaye. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: LUIS SUAREZ APASULIWA GOTI, YAELEZWA ATAPONA MAPEMA NA KUWAHI KOMBE LA DUNIA BADO BICHI KUANZIA MECHI NA ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top